MJUMBE WA NEC AISHANGAA CHADEMA KULINDA KURA KWA BASTOLA


Kulia Mjumbe wa Kamati kuu ya chama cha mapinduzi Goodfrey Mwalusamba (MNEC) akimnadi mgombea udiwani kata ya daraja mbili Philip Mushi Philip katika kampeni za uchaguzi mdogo

Kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya daraja mbili jijini Arusha zimeendelea kupamba moto huku kila aina ya vituko vikigubika chaguzi hizo ambapo Chama cha mapinduzi CCM kimetamba kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mdogo wa udiwani katika kata ya  daraja mbili jijini Arusha

Wananchi wa kata ya daraja mbili wakiwa makini katika kusikiliza sera za CCM.

Pia chama hicho kimerushia kombora kwa chama cha demokrasia na maendelo chadema kwa kusema kuwa watalinda kura kwa bastola huku wakishindwa kutumia majukwaa vizuri badala yake chama hicho kimekuwa kikitumia nafasi hiyo kutukana majukwaani

Akimnadi mgombea udiwani kata ya daraja mbili Mjumbe wa Kamati kuu ya chama cha mapinduzi Goodfrey Mwalusamba alisema bila kutaja jina la chama kuwa haina sera zaidi ya vitisho,matusi sanjari na vituko vya kila aina kwa madai kuwa watalinda kura kwa bastola

“Utaskia wanasema kuwa tuna Mungu huku wakidai watalinda kura na bastola ,,ndani ya CCM hakuna wanafki,wazushi watuonyeshe ni mangapi waliyoyafanya hadi sasa”alisema Mwalusamba
Kikundi cha masanja kikicheza ngoma

Aliongeza kuwa Nchi inaongozwa kwa misingi ya haki na sio vinginevyo huku akiwatahazarisha vijana kutokufata mikumbo ya hapa na pale na kunyweshwa pombea aina ya viroba ili wawatukane CCM huku akiwasihi watu kumpa kura Philip mushi ili kuharakisha maendeleo ya kata hiyo kwa kuwa wapinzani hao hawamtambui Meya wa jiji la Arusha

Naye mgombea wa udiwani Philip Mushi Philip alisema kuwa endapo watampa ridhaa ya kuongoza kata hiyo ni wazi kuwa atashughulikia mambo yafuatayo ikiwa ni ,kuboresha zahanati,barabara,mikopo kwa akina mama pamoja na vijana kujikita katika ujasiriamali

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post