JESHI LA POLISI LAMSAKA ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI LEMA


Mhe. Lema  Akiwa jijini London
 Jeshi la polisi mkoani Arusha linamsaka aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tuhuma za kushambulia mwili pamoja na upotevu wa simu pamoja na fedha.

Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa kamanda polisi Lebaratus Sabas alisema kuwa  jeshi la polisi linamsaka lema na wenzake ambao idadi yake hawajatajwa kwa tuhuma za kushambulia mwili wa watu wawili tukio lililofanyika october 28 mwaka huu katika kata ya daraja mbili.

Alisema kuwa jeshi la polisi lilipokea taarifa za malalamiko  kutoka kwa watu wawili waliojulikana kwa jina la Ibrahimu Juma pamoja na Maritin Daniel wote wakazi wa daraja mbili kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la arusha mjini Godbless Lema akiwa na wanzake walimvamia na kuwashambulia kwa ngumi pamoja na kuwanyanganya simu aina ya samsang yenye samani ya shilingi laki tatu pamoja na fedha taslim kiasi cha shilingi laki mbili kisha kuondoka na kuwaacha.

Alisema kuwa watu hao waliamua kutoa taarifa polisi na jeshi la polisi linamsaka lema kwa ajili ya kujibu tuhuma hizi .Lkibeneke la kaskazini lilimsaka lema  kujibu tuhuma hizi akupatikana kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa imezimwa.

1 Comments

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post