TUKIO LA KUKAMATWA KWA MTU ALIYEPATIKANA
NA SILAHA AINA YA RIFLE
MNAMO
TAREHE 13/10/2012 MUDA WA SAA 12:30 ASUBUHI, KATIKA KITONGOJI CHA NAKILONGOSI
KIJIJI CHA KAMWANGA WILAYANI LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOA WA ARUSHA
KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA HIFADHI YA TAIFA YA KILIMANJARO (KINAPA) WALIMKAMATA MTU MMOJA AITWAYE LONG’IDA S/O SILAYO (42) MKULIMA MKAZI
WA KAMWANGA AKIWA NA BUNDUKI AINA YA RIFLE
YENYE NO. 2758J KINYUME CHA SHERIA.
MAFANIKIO
HAYO YALIPATIKANA BAADA YA ASKARI HAO WALIOKUWA DORIA KUPOKEA TAARIFA KUTOKA
KWA RAIA WEMA AMBAYO ILIDOKEZA KUWEPO KWA MTU AMBAYE ANAJISHUGHULISHA NA
UWINDAJI HARAMU KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA KILIMANJARO NA ANAMILIKI SILAHA
KINYUME CHA SHERIA KWA MATUMIZI YA KUULIA WANYAMA AINA YA TEMBO.
KUFUATIA
TAARIFA HIYO NDIPO ASKARI WA JESHI LA POLISI NA ASKARI WA HIFADHI YA TAIFA YA
KILIMANJARO (KINAPA) KWA PAMOJA WALIKWENDA KUFANYA UPEKUZI KATIKA NYUMBA TATU ZINAZOMILIKIWA
NA MTUHUMIWA HUYO, AMBAPO WALIFANIKIWA KUIPATA
SILAHA HIYO NA YEYE MWENYEWE KATI
YA MOJA YA NYUMBA HIZO.
MARA
BAADA YA KUMKAMATA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LILIENDELEA KUMHOJI KUHUSIANA NA
UHALALI WA SILAHA HIYO NA YEYE MWENYEWE ALIKIRI KUIMILIKI ISIVYO HALALI KWA
KUWA HANA KIBALI CHOCHOTE KUHUSIANA NA SILAHA HIYO. MBALI NA SILAHA HIYO
KUITUMIA KATIKA MASUALA YA UWINDAJI HARAMU HAPA NCHINI NA NCHI JIRANI YA KENYA
PIA MTUHUMIWA HUYO AMEKIRI KUITUMIA SILAHA HIYO KATIKA MATUKIO YA UJAMBAZI
KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA HAPA NCHINI NA NCHINI KENYA.
MPAKA
HIVI SASA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUMHOJI MTUHUMIWA HUYO NA
ATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI WA AWALI KUKAMILIKA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
TAREHE 19/10/2012.