Umoja wa mataifa unasema kilimo cha bangi nchini Burma kimeongezeka kwa mwaka wa sita mtawalia.
Ripoti iliyotolewa na ofisi ya Umoja huo
inayoshughulikia masuala ya madawa ya kulevya na uhalifu inasemas sehemu
ya ardhi ambayo bangi hiyo imepandwa imeongezeka kwa asilimia kumi na
saba.
Umoja huo umelaumu ongezeka la ukuwaji huo wa
bangi kutokana na ukosefu wa utulivu na mzozo katika majimbo ya Shan na
kachin ambako ndiko kuna mashamba mingi ya bangi.
Inasemekana wakulima hawakuwa na mazao mbadala
ya kukuza kando na bangi hiyo ambayo hutumika kama kilewesha kwa kuwa ni
zao lenye faida kubwa kifedha.
Burma ni nchi ya pili duniani inayokuza kwa wingi bangi baada ya Afghanistan.
Mwandishi wa BBC anasema hakuna jitihada kamili
za kumaliza ukuwaji wa bangi kwa kuwa jeshi nchini humo na makundi ya
wanamgambo yananufaika kutokana na biashara hiyo.
chanzo bbc swahili