BREAKING NEWS

Monday, October 29, 2012

RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA SOPHIA AKUFFO KUFUNGUA MKUTANO UNAOWAKUTANISHA MAJAJI NA MABALOZI 54

Waziri wa sheria na katiba Mathias Chikawe akiwa na Jaji wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu kwenye ufunguzi wa mkutano wa shughuli za mahakama uliowashirikisha mabalozi kutoka nchi za umoja wa Afrika (AU) UNAONDELEA KWENYE UKUMBI WA HOTEL YA Mount Meru jijini hapa
majaji na mabalozi wanaoshiriki mkutano wa kufahamu shughuli za mahakama kutoka kwenye nchi za umoja wa Afrika akiwa katika matukio mbali mbali ya ufunguzi kwenye hotel ya Mount Meru


RAIS wa mahakama ya Afrika( Africa court) kutoka nchini Ghana  Sophia
Akuffo amefungua mkutano wa kamati ya kudumu ya umoja wa
Afrika(AU) uliokutanisha majaji  pamoja na mabalozi 54 kutoka nchi za
umoja wa afrika ulionza leo jijini Arusha.

Akifungua mkutono huo raisi wa mahakama ya Afrika Sophia Akuffo amezitaka nchi za bara la Afrika kuweka  muda na kutekeleza kwa vitendo na kuifahamisha jamii ya waafrika juu ya haki za binadamu na viongozi kuacha kukiuka haki hizo
.

Alisema kuwa  katika mkutano huo washiriki wataweza  kuangalia kwa
undani mahusiano yaliyopo kati ya mahakama ya kutetea haki za binadamu
pamoja na kamati ya wawakilishi ya umoja wa mataifa katika kuhakikisha
kuwa mahakama za afrika zinaboreshwa.

Aidha alisema kuwa mkutano huo utaweza pia kuunganisha ushirikiano
kati ya mahakama na mashirika mengine ya umoja wa afrika pamoja na
kamati ya kudumu ya wawakilishi wa umoja huo ili kuhakikisha kuwa
wanafanikiwa  katika mambo mbali mbali .

“mkutano huu  ni muhimu sana kwani majaji na mbalozi  wataweza
kujadili mambo mazuri ambayo yayawezesha hata mahakama kuondokana na
baadhi ya changamoto zinazowakabili”alisema Uwanone

Aliongeza kuwa  katika  mkutano huo wataweza kuweka mkakati  juu ya
Mahakama na kuweza kubuni njia mbali mbali  ambazo  zitaweza kulinda
haki za binadamu ndani ya  afrika.

Alieleza kuwa kamati ya wawakilishi ya kudumu ya umoja wa mataifa
itaweza kuweka umakini mkubwa kwenye mahakama  za Afrka kwa kuwa hiyo
ni moja ya sera zilizoko ndani ya umoja wa mataifa.

Hata hivyo mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbali mbali wa mahakama
ya haki za binadamu akiwemo makamu wa rais wa mahakama hiyo
,mwenyekiti wa kamati ya wawakilishi wa umoja wa mataifa pamoja na
muwakilishi wa kamati hiyo.
Habari na mahamod Ahamad wa libeneke la kaskazini

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates