WANAUME
HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII
Habari
za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi namshukuru Mungu kwa kuweza kunikutanisha na
nyinyi kupitia safu hii ambayo pamoja na mambo mengine nazungumzia juu ya mada
mbalimbali ambazo zinagusa maisha yetu ya kila siku.
Wiki
hii nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa.
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa
mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza
mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi
chote cha maisha.
Wanawake
wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata
wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie
wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali
sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura
nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao
nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa
nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika
mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo
ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
MWEYE
MAPENZI YA KWELI
Lengo
kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na
ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya
ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli
bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu
kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio
kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya
dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa
mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu
lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini
wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si
kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili
wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha
mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa
lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote
wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si
hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha
ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa
hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye
baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi
maisha ya raha mustarehe.
WENYE
TABIA NZURI
Tabia
njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni
katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu
cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo
wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani
utaambiwa anatabia mbaya. Naweza kusema
hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya
wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya
wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si
hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia
kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake
baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea
kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
WENYE
UCHU NA MAENDELEO
Hivi
karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi
hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa
hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za
kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa
wale ambao wako mijijini na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama
wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa
hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni
wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si
wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani
wafanye ili wafanikiwe.
WASIOPENDA
MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu
sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda
makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa,
kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?" Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki
tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,
"mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali
kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na
usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake
kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa.
Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na
pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda
lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia
akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’
hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani
ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume
ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho
watahitaji kama tu pesa haitakuwa
tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo
makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna
wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki,
anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine
wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi
kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba
ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano
wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa
na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha
ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.
WAVUMILIVU
Wapo
wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku
zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio
wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni
za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume,
huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea
kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama
nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu
kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza
hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na
atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya
starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha
ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu,
wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo
kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na
wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye
roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume
ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini
Dar-es-Salaam. Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue
kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa
umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza
yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza
kubadilika kwani inawezekana.