Njaa ni tatizo kubwa san
Mkutano unafanyika leo mjini London kujadili mkakati
a barani Afrikaati mpya wa utakaotumika baada ya ule wa malengo ya milenia.
Malengo hayo yaliwekwa mwaka elfu mbili
kuimarisha maisha ya watu katika nchi maskini na walitumai kuwa
yangefikiwa mwishoni mwa mwaka 2015.
Aidha malengo hayo yananuia kukabiliana na
maswala kama viwango vya umaskini, magonjwa , njaa na ukosefu wa elimu
lakini mafanikio yamekuwa kidogo sana ikilinganishwa na matumaini ambayo
watu walikuwa nayo.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron,
anafanya mazungumzo na Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Rais
Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia, wenyekiti watatu wa jopo la umoja
wa mataifa litakalopewa jukumu la kuweka mkakati mwingine mwaka 2015
kwa sababu ya malengo ya milenia.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wale wanaohudhuria
mkutano wa London watahitaji kutafakari ikiwa swala la malengo ya
kupata misaada ni wazo la kizamani liliopitwa na wakati.