JCB NA WENZAKE WASHIKILIWA TUHUMA ZA MAUAJI






Msanii wa muziki wa kufokafoka kutoka jijini Arusha jakobo makala (JCB) pamoja na wenzake watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za mauaji.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha lebaratus Sabas alisema kuwa msanii huyo pamoja na wenzake wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumpiga mwenzao hadi kufa katika ukumbi wa viavia sehemu ambayo walikuwa wanafanya shoo zao katika enyesho la jambo festaval lililokuwa likifanyika katika ukumbi huo.
Alisema kuwa marehemu huyo ambaye alitambulika kwa jina la Alex Julias Samweli(21) mkazi wa ilboru alihuzuria onyesho la Jambo Festaval lililokuwa likifanyika usikuwa wa october25 onyesho lililokuwa likifanyika katika ukumbi wa viavia jijini Arusha
Alisema kuwa katika siku ya tukio marehemu alikuwa mziki na wenzake ndipo alipopigiwa simu na watu wanaodaiwa ni pamoja na msanii huyu na wenzake  wakimtaka atoke nje ndipo alipo toka nje na aliporudi alionekana akitoka damu puani pamoja na kuwa na uvumbe sehemu za mwili.
"watu wa karibu waliokuwa na marehemu walipo muuliza kwanini amevimba na anatoka damu ndipo alipowajibu alitoka nje na kufanyiwa fujo na msaniii huyo akiwa na wenzake huku akibainisha kuwa  mbali na kufanyiwa fujo pia walimchulia simu yake ya kiganjani lakini alisema kuwa hajapata maumivu makubwa ila kadri muda ulipo zidi kwenda ndipo alizidi kuzidiwa na ndugu zake walimpeleka hospitali ya father babu  na kufariki akiwa hospitalini hapo"alisema kamanda sabas
Aidha aliwataja watu ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma hizi ni pamoja na msanii huyu Jacob Makala (JCB),Roberty Josephy(18) mkazi wa sekei,Sara Eprahimu(32) mkazi wa Engoshelaton pamoja na Remi Peter(22) mkazi wa unga LTD.
Alisema kuwa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya maunti meru na watuhumiwa wote wanashikiliwa na jeshi la polisi na pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post