BREAKING NEWS

Tuesday, October 23, 2012

WANANCHI WA MAKAMBAKO HATARINI KUKUBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KWA KUNYWA MAJI MACHAFU

hii ndo hali halisi

Wananchi wa halmashuri ya makambako wapo hatarini kukumbwa na magonjwa
ya mlipuko kutokana na kutumia maji yasiyo safi na salaama kutokana na
matumizi mabaya pamoja  na kutumia chanzo kimoja cha maji cha bwawa
lililopo katika mtaa wa mjimwema na uhuru makambako.

Wakielezea athali wanazoweza kupata wananchi hao wamesema baadhi ya
watu wanakwenda kutumia vyombo vya chooni,vingine vichafu ,kufua
pamoja na baadhi yao kuingia ndani ya maji wakati wa kuchota.

Pamoja na kulalamikia kukosa huduma hiyo ya maji katika mji mzima wa
makambako lakini wamesema maji yaliopo yanagawiwa kwa matabaka ambapo
tabaka la wananchi wa kawaida wanashindwa kupatiwa mgao wa maji huku
viongozi wa serikali wakiendelea kupata huduma hiyo ya maji karibu
kila siku.


Akizungumzia tatizo hilo mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa makambako
ambae pia ni diwani wa kata ya ubena Chesco Hanana Mfikwa amekili
kuwepo kwa tatizo hilo kwa mji mzima wa makambako na kwamba sababu ni
kutokana na kupungua kwa maji katika chanzo cha maji kilichopo
mtwango.

Kuhusu athali ambazo wananchi wa halmashauri hiyo wanaweza kupata
bwana Hanana amesema tayari serikali imeanza jitihada za kudhibiti
hali ya usal;ama wa chanzo hicho na kwamba baada ya wiki mbili
wanatarajia kuboresha bwawa hilo ili liweze kutoa huduma vizuri ya
maji kwa wananchi hao na kuwakinga kiafya tofauti na ilivyo kwa sasa.


Aidha Mfikwa amesema Hadi sasa wanapata maji kwa mgao huku akisema
halmashauri inatarajia kuongeza vyanzo vya maji kutoka
tagamenda,fukulwa na maeneo mengine yenye vyanzo vikubwa vya maji mara
tu badget ya fedha itakapokuwa imekamilika ili wakazi hao waweze
kutatuliwa tatizo hilo.

Hata hivyo amewataka wadau na wananchi wanatakiwa kuonesha ushirikiano
katika kutumia maji yaliyopo pamoja na vyanzo vyake visiharibiwe ili
kukabiliana na athali zinazowakabili kwa sasa za ukosefu wa maji hali
ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya wakazi wa halmashauri hiyo.

 Na Michael Ngilangwa wa libeneke la kaskazini Njombe

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates