Wafanyakazi
wa kiwanja cha ndege Pemba wamesema mapatao yanayopatika kiwanjani
hapo hayakidhi mahitaji ya kiwanja hivyo serikali kupitia wizara husika
wanahitaji kutupia macho na nguvu zao kiwanjani hapo.
Wamesema
hayo wakati walipotembelea na waziri wa miundombinu na mawasiliano Mhe
Rashid Seif ambapo wamesema kwa vile sasa wanatakiwa kubadilika
kiutendaji tokea kuundwa kuwa mamlaka kamili serikali haina budi
kuelekeza nguvu zao kiwanjani hapo ili kukifanya kiwanja hicho kuwa na
hadhi na haiba nzuri kwa wenyeji na wageni wanaotumia kiwanja hicho.
Aidha
wamesema mpaka saivi bado hawajaona mabadiliko yoyote tokea kundwa
mamlaka Jambo ambalo limekua likirudisha nyuma ufanisi wa kazi zao.
Hata
hivyo wamesema bado kama mamlaka wanafanya kazi katika mazingira magumu
sana hasa pale wanapofanya upekuzi mizigo ya abiria hulazimika kutumia
mikono na wala hawafahamu mizigo ile kama ipo salama ama laa.
Wafanyakazi
hao wamemuomba waziri huyo kufanya juhudi za makusudi kutafuta mashine
alau moja ya kupimia mizigo ya abiria ili waweze kugundua ndani ya
mizigo kuna kitu gani.
Aidha
wamemtaka waziri huyo kuchukua hatua maalumu kwa gari zinazoingia ndani
ya kiwanja kwani wamesema kuna baadhi ya gari zinazokuja kuchukua
viongozi huingia ndani ya uwanja jambo ambalo limekuwa likiharibu
barabara za ndege yaani( apron).
Kwa
upande wake waziri Seif amesema lengo haswa la kufanya ziara katika
taasisi mbali mbali za wizara yake ni kuangalia mapungufu yaliyopo ili
kuhakikisha mapungufu hayo yanapatiwa ufumbuzi yakinifu.
Aidha
Waziri seif aliwatoa wasiwasi wafanyakazi hao kuwa hakuna tofauti
katika ya kiwanja cha ndege unguja na cha pemba hivyo alimtaka meneja
msaidizi kuhakikiksha kuwa hudma zinazotolewa unguja lazima
Pemba ziwepo.
Sambamba
na hayo aliwataka wafanya kazi hao kubadilika katika utendaji wao na
wawe wabunifu ili waweze kujitangaza ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo uwanja wa ndege ni sehemu nzito ya kufanya kazi ambapo
alisema kila aliepewa dhamana ahakikishe anawajibika ipasavyo kwa vile
kazi ni sehemu ya maisha yao.
Baada
ya mazungumzo hayo mhe Waziri alitembelea jingo hilo kwa kukagua sehemu
ya choo ambavyo vimefanyiwa matengenezo, sehemu ya zima moto na
kuangalia mnara wa zantel ambao upo karibu na eneo la kiwanja hicho.
Na Nafisa Madai