WANAHABARI WALIOPATA SEMINA YA ONLINE JOURNALISM

Washiriki wa semina ya Online Journalism wakiwa katika picha ya pamoja na mkufunzi wa semina hiyo Lukelo Filex Mkami nje ya hotel ya Olasiti iliyopo jijini Arusha

Zaidi ya waandishi wa habari 20 wa mkoani Arusha wamepatiwa semina ya uandishi wa habari wa mtandao semina iliyofanyika kwa siku nne katika hoteli ya kitalii ya olasiti iliyopo jijini Arusha.

Wakizungumza katika semina hiyo baadhi ya waandishi hao ambao wamepata semina hiyo walisema kuwa wanaishukuru sana UTPC kwa kuwapa semina hii kwani wameweza kupata ujuzi ambao hawakuwa nao.
Mmoja waandishi hao aliyejitambulisha kwa jina la Ramathan Sywayombe alisema kuwa semina hii imeweza kumsaidia kujua jinsi ya kuandika habari za mtandano pamoja na jinsi ya kutengeneza  mtandao.
Alisema kuwa awali alikuwa anaona kuwa na mtandano au web site yake ni ngumu lakini kutokana na semina hii imeweza kumsaidia kupata ujuzi ziadi.
Semina hii ya ilianza kuma tatu na inatarajiwa kumalizika kesho  jijini hapa

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post