Kiongozi wa upinzani nchini
Rwanda Victoire Ingabire amehukumiwa miaka minane gerezani baada ya
kupatikana na hatia ya kosa la uhaini
Viongozi wa mashtaka walitaka afungwe maisha jela kwa kutishia usalama wa nchi.
Mahakama imempata na hatia ya kupuuza mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994.
Ingabire hakuwa mahakamani wakati hukumu
ilipotolewa dhidi yake kwani amekuwa akisusia kuhudhuria vikao vya
kusikilizwa kwa kesi hiyo akisema imeshinikizwa ksiasa,.
Mwandishi wa BBC mjini Kigali, Prudent
Nsengiyumva, anasema kuwa wakili wake, naibu kiongozi wa UDF, na baadhi
ya wafuasi wake, walikuwa mahakamani.
Walishangazwa sana na hukumu ya mahakama wakisema walitarajia angepata hukumu ya maisha jela.
Pia alikuwa anakabiliwa na tuhuma za ugaidi
lakini baadaye mahakama ilifutilia mbali wakati kesi yake ilipokuwa
inaendelea kwa miaka mwili.
Ingabire ana siku thelathini kukata rufaa.
Kiongozi huyo wa chama cha UDF, alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2010 na
alizuiwa kushuriki uchaguzi baadaye mwaka huo.
Bi Ingabire, ambaye ni mhutu, alirejea kutoka
uhamishoni nchini Uholanzi, mwezi Januari mwaka 2010 na amekuwa gerezani
tangu kukamatwa kwake.
Amekuwa akihoji kwa nini kumbukumbu za mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 hayajumuishi wahutu.
Zaidi ya watu waliofariki wakati wa mauaji hayo
walikuwa watutsi lakini pia wahutu wenye msimamo wa kadri waliuawa na
wahutu wenye msimamo mkali.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia