TIMU mbalimbali kutoka nchi za Kenya,Uganda na
wenyeji Tanzania zinatarajia kushiriki michuano ya Chipukizi Cup inayotarajia kutimua
vumbi kuanzia desemba 7 hadi 9 mwaka huu katika viwanja mbalimbali mkoani
Arusha.
Michuano
hiyo imeandaliwa na taasisi ya kukuza
vipaji vya soka nchini ya Future Stars Academy ambapo ina lengo la kukuza sekta
ya utalii nchini,kufahamiana,kukuza vipaji vya soka hususani kwa watoto wadogo.
Kwa mujibu
wa mkurugenzi na mwanzilishi wa taasisi hiyo,Alfred Itaeli alisema kwamba michuano hiyo itashirikisha
timu za wavulana walio chini ya umri wa miaka U-10,U-12,U-14 na U-17 huku timu
za wasichana zikiwa chini ya umri wa
miaka U-14 na U-17.
Itaeli,alisema
kwamba michuano hiyo itapigwa katika viwanja tofauti ambapo ni uwanja wa Sheikh
Amri Abeid,uwanja wa shule ya kimataifa ya Moshi sanjari na viwanja mbalimbali
vilivyopo mkoani Arusha.
Alizitaka
timu shiriki ikiwa ni pamoja na timu ya Alliance ya jijini Mwanza kuthibitisha
ushiriki wao mapema huku akiitaja ada ya
usajili kuwa ni $ 40 kwa kila timu
shiriki ambapo alisisitiza kuwa kutakuwa na zawadi ya vikombe na medali kwa
washindi wa timu mbalimbali.