HAFLA YA KUMUAGA KANAL MJENGWA DC MBINGA YAFANA SANA


Kutoka kushoto mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi,mkuu wa wilaya ya mbinga mstaafu Kanal Edmund Mjengwa,mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu,mkuu mpya wa wilaya Mbinga Senyi Ngaga na Mama Hanab Mwambungu wakigonga cheers wakati wa sherehe ya kumuaga Kanal Mjengwa jana mjini Mbinga.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Shaibu Mnunduma akigonganisha glass na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wakati wa sherehe ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa Wilaya hiyo Kanal mstaafu Edmund Mjengwa.
Askofu wa jimbo la Mbinga John Ndimbo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu jana mjini Mbinga wakati wa sherehe ya kumuaga Mkuu wa zamani wa wilaya ya Mbinga kanal mstaafu Edmund Mjengwa mjini Mbinga.
Mkuu wa zamani wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Kanal mstaafu Edmund Mjengwa akizungumza jana mjini Mbinga wakati wa sherehe yake ya kumuaga,katikati mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kulia mkuu mpya wa wilaya hiyo Senyi Ngaga.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post