MATOKEO YA AWALI YA UDIWANI MKOANI ARUSHA YAONYESHA CCM NA CHADEMA KUGAWANA KATA

Chama chama cha demokrasia na maendeleo chadema leo kimeweka kuibuka kidedea katika uchaguzi wa madiwani wa kata ya daraja mbili mara baada ya  mgombea wake Msofe Proper Remi kupata kura nyingi zaidi ya wagombea wenzeke

Katika uchaguzi huo wa kata ya daraja mbili ambao mwanzoni ulianza kwa fujo na jeshi la polisi kufanikiwa kuzituliza  na kuwakamata baadhi ya wananchi waliohusika na fujo hizo ambapo hadi gazeti hili liinaenda mtamboni idadi kamili yawaliokamatwa haijatambulika.

katika uchaguzi huu kulikuwa na wagombea watano ambao wametoka katika vyama vya siasa tofuti ambapokulikuwa na mgombea wa chadema ambaye ni Msofe Proper Remi,Zani Hassan Laizer kutoka  CUF,Wiliam Solomoni kutoka  TLP,Mohamed Adhumani Msuya kutoka NCCR pamoja na Philip Mushi Philipu kutoka chama cha mapinduzi CCM
katika uchaguzi huo ambao ulikuwa na jumla ya matawi 39 ya  kupigia kura pamoja na vitu vikuu viwili vya kuhesabia  ambapo kulikuwa na kituo cha daraja mbili shuleni pamoja na kituo cha filex mrema ambapo katika kituo cha filex mrema ndo sehemu ambapo ilifurika watu wengi walikuwa wakingojea matokeo
Kwa upande wa matokeo Chadema waliweza kuongoza kwa kura 2156,TLP kura 15,CCM 1282,CUF 22 na NCCR mageuzi kura nane
 kwa upande wa kata ya Bangata ccm waliweza kuongoza mara baada ya kupata kura nyingi zaidi ya wenzao ambapo  CCM  walipata kura 1177,huku CHADEMA 881na kwa upande wa TLP walipata kura 3

1 Comments

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

  1. tuambie uchaguzi ulifanyika katika kata ngapi na ccm tumeshinda katika kata ngapi na chadema nimeshinda kwa kata ngapi?

    ReplyDelete
Previous Post Next Post