Mwanasiasa wa Kenya Shem Kwega ameuawa huku mke wake akijeruhiwa mjini Kisumu Magharibi mwa Kenya.
Bwana Kwega alikuwa mshirika wa karibu wa waziri mkuu, Raila Odinga, anayegombea urais.
Polisi
waliwarushia gesi ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wanaelezea
kero lao kuhusu mauaji hayo wakidai kuwa yalikuwa mauaji ya kupangwa.
Hali ya taharuki inatanda nchini Kenya kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwezi Machi.
Zaidi
ya watu 1,000 waliuawa kwenye ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka
2007 zilizofuatia uchaguzi uliozua utata mkubwa kuwahi kushuhudiwa
nchini Kenya tangu uhuru.
Wiki jana
kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC, Fatou
Bansouda alielezea wasiwasi kuhusu tatizo la vurugu nchini humo.
Mahakama
ya ICC itawafungulia mashtaka washukiwa wanne wa ghasia hizo za baada
ya uchaguzi akiwemo naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta ambaye pia
anawania urais kwa kuhusika na ghasia hizo.
Bwana Kwaga na mkewe walipigwa risasi na washukiwa waliokuwa wanaendesha pikipiki.
Aidha marehemu Kwega alikuwa mfanyabiashara maarufu ambaye alikuwa anagombea kiti cha ubunge kwa chama cha waziri mkuu.
Ingawa
polisi wangali wanashuku kuwa huenda kilikuwa kitendo cha wizi, lakini
wafuasi wake wanaamini kuwa yalikuwa mauaji ya kupangwa