Wananchi wa kijiji cha kata
ya Kidegembye Wilayani Njombe
wamewakataa viongozi wa kata na kijiji hicho huku ofisi za viongozi hao za
kijiji na kata zikifungwa kwa muda wa
siku saba hadi leo bila kufanya kazi na kufunguliwa kwake hadi watakapo maliziwa
matatizo wanayokabiliwa.
Wakizungumza kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kijijini hapo mbele ya afisa taaraafa aliyekwenda
kusikiliza matatizo yao
kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba wamesema sababu za
kufunga ofisi hizo ni kutokana na hujuma za mali za kijiji zilizofanyika na
uongozi wa kijiji na kata hiyo ikiwemo kutowa somea hesabu za mapato na
matumizi ya michango ya shule ya sekondari Kidegembye kwa muda wa miaka mine
sasa.
Aidha wananchi hao wamesema
mbali na hayo sababu nyingine iliyowafanya waukatae uongozi wao wa kata na
kijiji kuwa ni pamoja na diwani wao kuhujumu michango ya wananchi ya ujenzi wa
madarasa na kuendeleza majengo ya shule ya sekondari kidegembye akiwa mwenyekiti wa bodi ya shule.
Halikadharika madai mengine
ya wananchi hao ni kwamba diwani wa kata hiyo amekuwa akitumia madaraka vibaya
kwa kuwanyang’anya mali zao zilizopo mpakani mwa shule ya sekondari kidegembye
kwa kupitia mgongo wa shule hiyo kwa maslahi binafsi,kutumia mfumo wa
kidikiteta katika utawala wake,ahadi za uongo, ,huku mtendaji wa kijiji akiwa
mlevi kupindukia hali iliyomfanya apoteze kitabu cha ushuru,kuhusika na wizi wa
mawe na kuwalea na kuwalinda vijana wezi
.
Pamoja na hayo wananchi hao
wamesema kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji hicho wanamutuhumu kwa kosa la
kushindwa kusimamia na kutetea haki na mali za wananchi pindi wanapovamiwa
katika maeneo yao,kushindwa kutambua kuwatawala
kimaadili,kanuni na sheria za uongozi kwani amekuwa akitawaliwa na
diwani pamoja na mtendaji wa kijiji hicho.
Sanjali na hayo wananchi hao
wamesema kuwa kutokana na matatizo walioyaodhesha hapo juu ilipelekea kufunga
ofisi hizo huku wakibainisha baadhi ya viongozi wa wa kata na vijiji kuwa
hawastahili kuendelea kutawala kijiji hicho akiwemo diwani na mwenyekiti wa
bodi wa shule ya sekondari
kidegembye,mwenyekiti wa kamati ya ujenzi na baraza la kata yote huku katika
ngazi ya kijiji akiwemo mtendaji wa kijiji hicho na wajumbe wake.
Kwa mujibu wa taari yao wananchi hao mbele ya afisa taarafa iliyosomwa na
Batwel Ngewe kwa niaba ya wananchi wote hawatakuwa tayari kufungua ofisi hizo
endapo viongozi hao wataendelea kuwepo madarakani huku wakisema wanapoondoka
madarakani wakabidhi mali
zao walizopolwa.
Afisa taraafa wa Lupembe
bwana Baltazary Mveyange amekili kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafikisha
kwa mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba ili kulifanyia ufumbuzi tatizo la wananchi hao
huku akisema taarifa zinazowafikia viongozi wa ngazi za juu ni tofauti na malalamiko yanayotolewa na
wananchi hao.
Aidha Afisa tarafa huyo
Mveyange amesema taarifa zilizotolewa na viongozi wa kata na kijiji hicho cha
kidegembye ni kwamba wanaolalamikia kunyang’anywa na kudhurumiwa haki zao ni
kikundi cha watu pekee lakini amekili kuwepo kwa mapungufu ya viongozi wa kata
na kijiji hicho huku diwani wa kata hiyo akishindwa kuhudhuria mkutano huo
na simu yake haipatikani licha yakupewa
taarifa mapema.
Mkutano huo umeahirishwa hadi
wiki ijayo mara uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe akiwemo mkuu wa
wilaya ya Njombe na mkuu wa shule ya sekondari kidegembye ambapo watakwenda
kushuhudia maeneo yanayolalamikiwa na kusema wakati wowote katikati ya wiki
watapewa taarifa juu ya ujio wa wawageni hao.
Hadi sasa viongozi wa kata na
kijiji cha kidegembye mkoani Njombe wanatimiza siku ya saba bila kutumia ofisi
za kijiji na kata kutokana na wananchi hao kufunga ofisi hizo huku wakipeana
zamu ya kulinda wakati wa usiku na mchana ili ofisi hizo zisipatwa na tatizo
la kuvunjwa mpaka ufumbuzi utakapo
patikana.
Habari hii imeandikwa na mdau wa libeneke Johnson Mwombeki kutoka mkoani Njombe
Hongera kwa kazi mnayo ifanya kwa kutuwakilisha watu wa kidegembye kwa habari motomoto.
ReplyDelete