WAZAZI PAMOJA NA WALEZI WATAKIWA KUTHAMINI SHERIA KULIKO ELIMU YA WATOTO WAO





Mkurugenzi wa shule ya Arusha Modern, Khalfan Saidy Masoud alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwaondoa hofu wananchi na wazazi wenye mapenzi mema na watoto wao juu ya kuwapa urithi bora wa elimu kuwa shule hiyo haijauzwa kama inavyodaiwa bali yaliyouzwa ni majengo tu



wazazi na walezi kote nchini wametakiwa kuwa msatari wa mbele na kuona umuhimu wa kuwekeza katika elimu kwa watoto wao kama wananyowekeza fedhe nyingi katika katika sherehe mbalimbali.


Rai hiyo imetolewa na makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seph Ally Iddy alipokuwa akihutubia kwenye mahafali ya kumi ya shule ya Arusha modern(Arusha modern school) mapema leo shuleni hapo.


Balozi Seph ambaye pia alikuwa mgeni Rasmi katika mahafali hayo alisema kuwa watu wa sasa wanapenda kuwa mstari wa mbele katika kuchangia fedha nyingi kwenye maharusi, ubarikio, send-off, birthday, n.k lakini wanakuwa wagumu kuchangia watoto wapate elimu bora ambayo ndiyo itakuwa urithi pekee kwa mtoto hapo baadae.


"Watu sasa hivi wanafurahisha sana mtu ukimwambia achangie gharama za mtoto wake au wa jirani yake au ndugu akapatiwe elimu nzuri wanaanza kupiga mahesabu ya hizo hela lakini hapigi mahesabu kwa mwaka amechangia shilingi ngapi kwenye sherehe mbalimbali za watu ambao hata hawamfahamu, huo ni uzamani hebu twende na wakati kwa kuwapeleka watoto wetu shule kwani huo ndio urithi pekee kwao hapo baadae.


Awali mmiliki wa shule hiyo ya Arusha Modern, mwalimu Khalfan Saidy Masoud akielezea changamoto za kielimu wanazokumbana nazo shuleni hapo alisema kuwa ni baadhi ya wazazi kushindwa kulipa ada za watoto wao kwa wakati na wengine kufikia hadi kuwahamisha watoto wao kabla ya kuhitimu masomo.


Mwalim Masoud pia aliwaondoa hofu wazazi wenye watoto wao shuleni hapo na wananchi wote kwa ujumla wenye malengo mazuri ya kuwekeza elimu kwa watoto wao kwa kuwapeleka shuleni hapo juu ya tetesi za shule hiyo kuuzwa,

"naomba nifafanue usemi wa watu kusema shule hii imeuzwa, si kweli shule imeuzwa, iliyouzwa ni majengo tu lakini menejiment nzima ya shule na taaluma iko pale" alisema mwalimu huyo na kuongeza,

"Tumeamua kuuza majengo haya kutokana na ufinyu wa eneo hivyo tunahamia njiro ambako tumepeta eneo kubwa na la kututosha kulingana na mahitaji lengo ikiwa ni kuberesha elimu tunayoitoa inayokwenda na wakati wa sasa wa kimataifa" alimaliza mwalimu Masoud.


Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo, Philip Wasike aliwataka wahitimu wote hasa wa kidato cha nne na sita kujitambua kuwa wao sasa ni wasomi hivyo watilie maanani yale waliyofundishwa shuleni hapo kuwa faida kwa jamii na taifa kwa ujumla sambamba na kuona umuhimu wa kujiendeleza kielimu siyo kukimbilia maisha kwani yapo na watayakuta.


Alisema kuwa shule hiyo ina wanafunzi kutoka nchi 12 duniani ambapo leo wamehitimu wanafunzi 130 kwa ngazi tofauti tofauti ambapo kidato cha sita wamehitimu 19, na kidato cha nne 16 huku darasa la saba wakihitimu 27.


Hawakuishia hapo pia walikuwepo wanafunzi maalum wa kidato cha tatu 40 walihitimu ambapo hawakuwasahau pia waliohitim darasa la awali la chekechea (baby class) ambapo walihitim 27 na mwakani wanaanza kufurahia masomo yao ya shule ya msingi (darasa la kwanza).

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post