WOMEN IN BALANCE, KITCHEN PARTY GALA YAWAPA ELIMU UNYUMBA WANAWAKE JIJINI DAR


Msemaji katika Hafla ya Women in Balance Kitchen Party Gala Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Chris Mauki akitoa somo la Saikolojia kwa wakinamama na wasichana waliohudhuria hafla hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall jijini Dar.

Life Style Designer of Sex and Relationships kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai akitoa somo la kuhusiana na masuala ya mahusiano ya kimapenzi kwa wenye ndoa na wasiokuwa na ndoa ambapo amesema vipo vitu vingi vinavyochangia kuboresha ama kuharibu mahusiano hayo ambapo wahusika wanatakiwa kuvifahamu na kuvitilia mkazo ili kudumisha mahusiano yao.

Mafunzo kwa vitendo yalihusika pia.
Msemaji wa mwisho alikuwa ni Mama Veronica aliyewaacha hoi kwa vicheko wanawake waliohudhuria Kitchen Party Gala ambapo alizungumzia masuala ya uvumilivu katika ndoa sio tu kukosekana kwa kipato ndani ya nyumba bali hata mikimiki ya Unyumba kwa wanandoa.
Independent Sales Consultant wa bidhaa za Oriflame Bi. Jesca Mwakyulu akionyesha bidhaa ya Feminele Intimate Wash ya Oriflame ambayo ameisifia kuwa na Natural Lactic Acid ambayo inasaidia kutunza hali halisi ya sehemu za siri za Mwanamke.
Amefafanua kuwa kwa asili sehemu hizo zina hiyo Lactic Acid ambayo hutunza unyevu sahihi na Bacteria wazuri ambao husaidi kutoa ulinzi dhidi ya Fangasi, miwasho na harufu mbaya.
Mmoja wa wadhamini wa Women in Balance Kitchen Part Gala Mwakilishi kutoka TSN Super Market Lizbeth akitangaza zawadi kumi kwa wageni waliohudhuria Kitchen Party Gala zikiwemo Vocha za kufanya Shopping katika Super Market za TSN zilizopo jijini Dar es Salaam.
Wakinadada wakionekana kufurahishwa na mambo yaliyokuwa yakizungumziwa kwenye Kitchen Party Gala hiyo.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Juhyna Kusaga (kushoto) na mdogo wake.
Mbunifu nguli wa mavazi nchini Khadija Mwanamboka (kulia) a.k.a Kubwa la maadui alikwa miongoni mwa waliohudhuria Women in Balance Kitchen Party Gala.
Women in Balance Kitchen Party Gala ilikusanya wakina mama na kina dada kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya nje kama inavyoonekana picha na hii kudhihirisha jinsi gani wakimama wanavyopenda kupata Elimu ya kudumisha ndoa zao na familia kwa ujumla.
Palikuwa hapatoshi hakuna hata pakuhemea.
What a beautiful smile.
Salma Msangi wa Channel Ten na Magic Radio.
Mratibu wa Women in Balance Kitchen Party Gala Dina Marios akiteta jambo na Mama Veronica.
Vicheko, nderemo na vifijo vilitawala.
Aunty Sadaka na Mwanasaikolojia Chriss Mauki.
Warembo katika pozi mbele ya Camera yetu.
Skylight Band walikuwepo kutumbuiza Hafla hiyo. Uzao wa Bongo Star Search Mary Lukas akitoa burudani.
Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kali kukonga nyoyo za kinamama waliohudhuria Women in Balance Kitchen Party Gala.
Blogger Shamim Mwasha (kushoto) a.k.a Zeze wa 8020 Fashions katika pozi na Mshehereshaji wa Women in Balance Kitchen Party Gala Gea Habib.
Mratibu wa Women in Balance Kitchen Party Gala Dina Marios (kushoto) na Mgeni wake kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai.(Picha zote na Zainul Mzige).

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post