Msaidizi wa
Balozi wa Tanzania nchini Italia,Mh. Salvator M.J. Mbilinyi akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italia
na baadhi ya wajumbe
Jumuiya ya Watanzania Italy iliandaa mkutano
Msaidizi
wa Balozi wa Tanzania nchini Italia,Mh. Salvator M.J. Mbilinyi
akizungumza machache wakati wa mkutano wa viongozi na wajumbe kwa ajili
ya kuweza kutoa ufafanuzi kwa
Watanzania walio ughaibuni kushiriki kuchangia maoni ya upatikanaji wa
katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jumuiya
ya Watanzania Italy iliandaa mkutano wa viongozi na wajumbe kwa ajili
ya kuweza kutoa ufafanuzi kwa Watanzania walio ughaibuni kushiriki
kuchangia maoni ya upatikanaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mkutano
huo uliofanyika siku ya ijumaa tarehe 19/10/2012 ulihudhuriwa na Mh.
Salvator M.J. Mbilinyi msaidizi wa Balozi na mkuu wa utawala kutoka
ubalozi wa Tanzania Rome Italy kama mgeni rasmi. Naibu balozi alianza
kwa kuwapongeza Watanzania Italia kwa mchango wao mkubwa kwa taifa.
alisema
kwa kuwa serikali inatambua mchango wa Diaspora ya Watanzania, ndio
maana umewekwa utaratibu huu kwa walio ughaibuni kuweza kutoa maoni
katika upatikanaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mchakato
wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka
kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume ambayo ni
www.katiba.go.tz Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa
ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa
kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya. "Mh
Mbilinyi alinukuu muongozo uliotolewa na tume ya katiba.
Mh Mbilinyi alielezea pia mambo muhimu ya kuzingatia katika kuchangia maoni kwa Watanzania walioko ughaibuni "alisema
Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
Mtu
yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki
katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini
amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo
atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.
Pia
alieleza njia tatu za ukusanyaji maoni, alisema njia tatu za ukusanyaji
wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama zifuatazo:
(i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti
(www.katiba.go.tz) barua pepe ya Tume, ( katibu@katiba.go.tz This e-mail
address is being protected from spambots.
nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769
(ii)
Utoaji
wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani
ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681
DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
Endapo
Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa
ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama
Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya
maoni iliyoandaliwa na Tume.
Mwisho
Mh Mbilinyi alielezea kuhusu utambulisho wa mtumaji maoni kuwa kila mtu
atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv) endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi
yake (ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).
Tume
inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la
uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu
raia wa Tanzania pekee. Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia
ndugu Abdulrahaman A.Alli aliwashukuru viongozi na wajumbe wote na
kuwataka kufikisha salam hizi kwa Watanzania wote ili kila mtu atumie
haki hii muhimu ambayo ni mchango mkubwa wa taifa letu.
Jumuiya
ya Watanzania Italia inategemea kuandaa mikutano mingine mjini
Modena,Genova, Roma na sehemu nyingine ambako kuna Watanzania kwa
madhumuni kama haya ya kuhamasisha na kutoa ufafanuzi juu ya uchangiaji
maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwandishi: Kagutta N.Maulidi (Blogger)