Msanii wa kike raia wa Sweden aishiye nchini, Saraha amesema Bongoflava ndio muziki pekee aliotokea kuupenda zaidi na kwamba ni muziki atakaokuwa akiufanya muda wote.
Saraha ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha Enews cha EATV.
Pia alielezea kuhusu kukamilika kwa albamu yake aliyoipa jina la ‘Mbele Kiza’ ambayo ina nyimbo kama Jambazi.
Hivi karibuni mume wake ambaye ni producer wa Usanii Production, Fundi Samweli alitangaza kuwa yeye na Saraha watarajea nchini kwao Sweden kuendelea na shughuli zao huko.