Na. Mwandishi wetu.
Makampuni matatu makubwa yaliyo ndani ya MeTL Group hivi majuzi yamefanikiwa kutwaa tuzo za Rais za Watengenezaji Bidhaa kwa mwaka 2013.
Makampuni hayo ni: East Coast Oils & Fats Ltd ya Kurasini ambayo hutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia pamoja na bidhaa nyingine.
Afritex Limited ambayo hutengeneza Khanga, Vitenge na bidhaa zifananazo; na 21st Century Textiles ambayo ni kampuni kubwa na ya kisasa Afrika Mashariki na kati inayotengeneza bidhaa kama khanga, vitenge, vikoi, mashuka, nguo za kimasai n.k.
Tuzo ya Rais ya Watengenezaji wa Bidhaa ni tuzo ambayo hutolewa kwa makampuni mbali mbali nchini Tanzania yanayojihusisha na utengenezwaji wa bidhaa. Ubora wa bidhaa ndio hufanya kampuni kushinda tuzo hiyo.