Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwanafunzi Happnes John wa shule ya sekondari motamburu moja ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu kwa shule ya sekondari Motamburu iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro. |
Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwalimu mkuu(Abel Masuki kushoto) wa shule ya sekondari motamburu baadhi ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu shuleni hapo. |
Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Program yake ya shule
yetu imeendelea na zoezi lake la kuinua kiwango cha ufaulu katika
masomo ya sayansi ambapo imekabidhi vitabu vya ziada na kiada katika
masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari ya MOTAMBURU iliyopo Kata
ya tarakea wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia
msaada huo Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone
Majwala alisema" program ya shule yetu inayolenga kutoa vifaa vya
kufundishia mashuleni ikiwemo vitabu vya kiada na ziada kwa upande
wa masomo ya sayansi ambapo mpaka sasa wameweza kufikia shule 900
katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani ".
"Tutaendelea
kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha
tunaboresha elimu mashuleni na kupunguza changamoto za upatikanaji wa
vitabu katika shule nyingi nchini. sliongeza Majwala
Mkuu
wa wilaya ya Rombo Elinasi Pallangyo ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi
katika hafla fupi za makabidhiano hayo ,alipokea msaada wa vitabu na
kuukabidhi kwa uongozi wa shule baada ya kukabidhiwa na meneja biashara
wa Airtel kanda ya kaskazini ambapo amewashukuru airtel kwa msaada huo
ambao amesema umekuja wakati muafaka huku akiwakumbusha wadau wengine
kuiga mfano wa Airtell Katika kuchangia maswala muhimu ndani ya sekta ya
elimu hususani katika maeneo ya vijijini.
Akitoa
taarifa fupi ya maendeleo ya shule kwa mkuu wa wilaya mkuu wa shule
ya sekondari MOTAMBURU Abel Masuki ameishukuru airtel Tanzania kwa
msaada huo ambao wamesema Airtel imeonyesha kuwa mfano mkubwa kwa
makampuni mengi kwa kuungana na serikali kutekeleza sera ya elimu ya
kuwaelimisha watanzania wengi hasa walio maskini kuwaondolea ujinga
lakini pia akatoa changamoto ya vifaa vya maabara.