Mwanamuziki wa pop asiyehishiwa vituko
kila kukicha, Lady gaga ametoa mpya baada ya kuvaa nguo iliyomuacha
wazi sehemu kubwa ya mwili wake kiasi kwamba unaweza ukaona kila kitu
alichovaa kwa ndani wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa
kutimiza miaka 28 iliyofanyika katika ukumbi wa ‘Roseland Ballroom’ New
York Marekani
”Asanteni sana kwa kujumuika na mimi
kwenye bethidei yangu, nilipoamka asubuhi nilikuwa na furaha. Nilikuwa
nahamu ya kuwepo hapa usiku huu. Nina marafiki wengi hapa..mashabiki
wengi na nimekulia kwa miaka sita” alisema Gaga