Ofisa
Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo
akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhisina na uzinduzi wa upimaji
macho utakao fanyika Dar es Slaam free market mkabala na kituo cha DSTV ,
Kinondoni jijini Dr es Salaam. Kushoto ni Mratibu mradi huo Violet Shirima.
Ofisa
Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo akionesha miwani itakayozinduliwa.
********
MKUU wa Wilaya ya
Kinondoni, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa
utoaji wa huduma ya macho bure, itakayofanyika Dar es Slaam free market mkabala
na kituo cha DSTV , Kinondoni jijini Dr es Salaam.
Ofisa Mkazi wa
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo alisema hayo
jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema wameamua
kutoa huduma hiyo bure kwa sababu inakadiriwa, watanzania Milioni 3.5
wameathirika na ugonjwa wa macho wengi wao ni wenye umri wa miaka 40 na
kuendelea.
Alisema huduma
hiyo itaanza kutolewa leo hadi Aprili 11 mwaka huu jijini Dr es Salaam,
kuhamasisha watu kuwa na desturi ya kupima macho mara nyingi zaidi.
‘’Tumeandaa
miwani za aina 12 ambazo saizi zote zinapatikana na tutaziuza kwa bei nafuu
kuliko wanavyouza mawakala wengine’’ alisema Mashayo.
Aliongeza kuwa
Taasisi hiyo inatoa huduma katika mikoa nane ambayo ni Mbeya, Mwanza, Mtwara,
Singida, Iringa, Dodoma, Songea na Lindi.