KIJAZI AWATAKA WATANZANIA KUTEMBELEA VIVUTIO
Watanzania wametakiwa kuvipenda vivutio vya utalii na kujenga mazoea ya kuvitembelea kwani ni urithi waliojaaliwa na mwenyezimungu na kuvithamini sanjari na utunzaji wa vivutio hivyo kwani ni njia ya kuwapatia maendeleo na ajira itakayolipaitia taifa letu maendeleo endelevu kwani sekta hiyo inakuwa kwa kasi siku hadi siku.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa shirika la hifadhi za taifa (TANAPA)Allan Kijazi wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la kimataifa la utalii(UNWTO) linaloendelea jijini hapa jana na kutanabaisha kuwa sekta hiyo imekuwa na changamoto nyingi katika ukuaji wake ikiwemo njia za kuitangaza kimataifa na hapa nchini hili limekuwa ni tatizo kwa kuwa bado watanzania hawajajitokeza kuinga mkono sekta hiyo kwani hawajajenga mazoea ya kutembelea vivutio hivyo.
Kijazi alisema kuwa ilikuwa na uchumi endelevu kwenye sekta ya utalii tunahitaji kufuta sheria ya taifa ya ukuaji wa uchumi ya mwaka 2004 kwa kuwekeza kwenye sekta hiyo ili kuweza kutupaita kipato cha kujenga taifa na wananchi waweze kupata faida ya kiuchumi kutokana na rasilimali zao waliojaaliwa na mwenyezimungu kwa kushirikiana kwa pamoja na mashirika mbali mbali ya uwekezaji tunaweza kufikia malengo endelevu kwenye bara letu la Afrika.
Aidha alisema kuwa ilikuwa na nguvu ya kuyafanya haya yote tunahitaji kuunganisha nguvu kwenye mipango endelevu ya kuutangaza utalii wa ndani na nje ya nchi zetu na kutolea mfano wan chi zilizopiga hatua kama South Afrika,na Botswana kwani nchi yetu kwa sasa inaelekea huko tuandae miundo mbinu itakayowafanya watalii kupenda kuja kutembelea vivutio hapa nchini na kwenye bara letu.
“Bara letu limejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii hivyo ni wakati muafaka kuvitangaza na kutumia rasilimali zetu kujenga uchumi wan chi zetu kwani makadirio ya watalii yanaanza kutuzidi huku uwekezaji kwenye sekta hiyo ukiwa bado chini”alisema Kijazi
Kijazi alisema kuwa mazingira ya vivutio vyetu yanavutia kwa watalii na kuwa ni sehemu ya kuendesha uchumi wa nchi yetu hivyo tunakila sababu ya kujivunia kuwa watanzania na kuendelea kuvitangaza vivutio hivyo popote ulimwenguni bila ya kusubiri kuwa kazi hiyo ni ya serekali pekee.
Nakuwataka watanzania wakiwemo vijana wa mashuleni kuanza kujenga mazoea ya kutembelea vivutio hivyo huku akitanabaisha kuwa si kuvisoma kweny vitabu pekee bali kusoma nadharia na vitendo hii ndiyo njia ya mwanzo ya kukuza utalii wa ndani ya nchi yetu na taifa litaendelea kunufaika kiuchumi na uchumi ukitengamaa utarudi kwa watanzania.
|
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia