MAELFU YA WATU WAKUSANYIKA SHEIKH AMRI ABEID KUIOMBEA NCHI YETU
MAELFU ya wakazi wa jiji la Arusha walikusanyika
katika kongamano lililofanyika katika viwanja vya kumbukumbu wa sheikh amri
Abeid ili kuvunja maagano pamoja na kuiombea nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania ili iweze kuondokana na madeni.
Akizungumza katika
viwanja hivyo Mtumishi wa Mungu Christian Mwabukusi alesema kuwa mfululizo wa
maombi hayo ni kuvunja maagano mbalimbali ili kuweza kumuomba Mungu ili aweze
kulinusuru taifa haswa katika madeni ya kurithi.
Bw.Mwabukusi
alisema kuwa inabidi yafanyike maombi ya kuvunja maagano ili kuweka maagano
mapya katika ulimwengu wa roho ili Mungu
aweze kusamehe na hatimaye nchi iweze kuwa na neema na kuondokana na madeni.
Alisema kuwa
lengo ya kongamano hilo ni kuweka agano
la uzima na uhai ili watu waweze
kufurahia maisha na kuondokana na mizigo ya madeni na magonjwa mbalimbali.
“Unajua kuna
vitu vinafanyika katika ulimwengu war oho mfano kama rais wa kwanza aliondoka
akaacha madeni utakuta rais atakeyekingia madarakani naye pia anaridhi madeni
hatimaye taifa pia linaingia katika mrundikano wa madeni hivyo katika ulimwengu
wa roho ni lazima maombi hayo yawezekufanyika ili kuvunja maagano na roho
za madeni”alisema bw.Mwabukusiha
Aidha alifafanua
kuwa mbali na kuvunja maagano pia wananchi hao wa madhehebu mbalimbali wamepata
fursa ya kuiombea nchi iwe na amani ikiwa ni pamoja na uchumi wan chi kukua ili
wananchi waweze kupata maendeleo.
Alisema kuwa
faida ya kuvunja agano ni kupata uzima ambapo pia mtu anaweza kuishi maisha kwa
raha na kuondokana na mizigo ikiwa ni kudumu katika amani ambamo ndani yake
kuna maendeleo ya kiuchumi,kijamii na maendeleo ya kimwili ili kuondokana na
magonjwa mbalimbali.
Maombi hayo yameshirikisha
maelfu wa wakazi wa Jiji la Arusha,Mwanza,Tanga,Dar es Salaam,Manyara na
Kilimanjaro ambapo yameandaliwa na kituo cha radio na maombi cha Safina
kilichopo katika Kata ya Kaloleni jijini Arusha.
Habari na mdau wa libeneke Ashura Mohamed,Arusha
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia