CCM CHALINZE YAZIDI KUBOMOA NGOME ZA WAPINZANI

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye sambamba na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete wakiyarudi magoma wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika Kijiji cha Lugoba,Kata ya Lugoba.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia Mamia ya wakazi wa Kijiji cha Lugoba waliofurika kwenye uwanja wa Mnadani,kusikiliza sera ya Mgombea Ubunge huyo
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lugoba wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,leo April 2,2014.
Mbunge wa Jimbo la Mchinga,Said Mtanda akihutubia wakazi wa Lugoba na wananchi wa Chalinze kumchagua Ridhiwani Kikwete ili waweze kushirikiana nae katika kuendeleza maendeleo ya Jimbo hilo.
Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi akiwapa maneno murua kabisa wananchi wa Kata ya Lugoba na kuwataka waache kwenda kujiunga na vyama vingine,kwani maendeleo ya kila Mtanzania yanaletwa kupitia CCM.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
Bi. Mwanahawa Omary aliekuwa Mwanachama wa Chadema akirudisha kadi kwa Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akiiangalia kadi ya CHADEMA ya Mzee Masoud Mtonga mara baada ya kukabidhiwa.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea kadi za Chama cha CUF kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kata ya Msata,Idd Njema ambaye amejiunga na CCM sambamba na familia yake.katikati ni Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kata ya Msata,Idd Njema akizungumza machache muda mfupi baada ya kujiunga na CCM.











Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post