Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Paul
Sarakikya,Akiongea na waandishi wa habari jiji Arusha
waandisi wa habari wakiwa wanamsikiliza kwa makini kaimu mkurugenzi wa idara ya wanyama pori
JUMLA
ya meno ya tembo 495 yamekamatwa kwenye maeneo mbalimbali nchini katika kipindi
cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
Aidha
watuhumiwa wa ujangili 544 wamefunguliwa mashitaka kwenye mahakama mbalimbali
ambapo kesi 62 zimemalizika huku 38 zikiwa bado zinaendelea.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Paul
Sarakikya, alibainisha hayo mjini hapa jana alipokuwa akitoa taarifa ya robo
mwaka juu ya hali ya ujangili nchini.
Alisema
kuwa nyara hizo za serikali zilikamatwa kutokana na doria iliyoendeshwa na
watumishi wao waliopo kwenye mapori ya akiba na kikosi cha kuzuia ujangili
kwenye maeneo mbalimbali.
Sarakikya
alisema kuwa katika kipindi hicho, jumla ya mizoga ya tembo 39 ilionekana ndani
na nje ya hifadhi za taifa na mapori ya akiba huku nyama za wanyamapori kilo
1,111 zikikamtwa.
“Aidha
meno ya tembo yaliyokamatwa yalikuwa katika hali mbalimbali ambapo mazima
yalikuwa 171, vipande 22 vya meno ya tembo ghafi, vipande 302 vya meno ya tembo
yaliyochakatwa yenye jumla ya kilo 662.62 yalikamatwa,” alisema.
Alisema
kuwa pia walifanikiwa kukamata silaha 11 ikiwemo bunduki ya rasharasha 1, rifle
3, shotgun 2, gobore 5 pamoja na risasi saba za aina mbalimbali.
“Mali
na vifaa vingine vilivyokamatwa ni pamoja na magari matano ambavyo vilikamatwa
kwa kuhusika kwenye vitendo vya ujangili hasa wa meno ya tembo, ng’ombe 2,663
walioingia kwenye hifadhi pamoja na msumeno mmoja wa kukata mbao na mbao 745,”
alisema Sarakikya.
Alisema
kati ya kesi 124 zilizofunguliwa kwenye mahakama tofauti nchini, 62 zilizokuwa
na washitakiwa 85 zilimalizika kwa watuhumiwa kulipa faini ya zaidi ya sh
milioni 25.5.
Sarakikya
alisema meno ya tembo waliyokamata yalitokana na matukio ya siku za nyuma,
jambo alilodai walilibaini kutokana na meno hayo kuwa yamebadilika rangi kwa
kuchimbiwa ardhini muda mrefu huku mengine yakimeguka.
Taarifa
hii imekuja siku moja baada ya watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majangili
kukamatwa na meno ya tembo 53 yenye jumla ya kilo 169.7 wakiwa na silaha aina
ya SMG yenye magazine tatu kwenye Kijiji cha Kiomboi wilayani Manyoni mkoani
Singida.