Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Uingereza Bw. Hague alipomtembelea ofisini kwake jijini London kwa
mazungumzo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza
Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini
London kwa mazungumzo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi mpango wa
bima ya afya na maafa wa WESTADI wa mfuko wa Jamii wa NSSF jijini
London, akiwa na Mkurugenzi wa NSSF Dkt RAmadhani Dau na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo Bw. Abubakar Rajabu (kushoto) . Mwenye
miwani kati ni Bw. Aboubakar Faraji aliyekuwa mwongoza sherehe wa siku
hiyo ambapo Dkt Kikwete alikutana na kuzungumza na Watanzania waishio
Uingereza.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyabishara wakubwa na
wawekezaji wa Uingereza aliokutana nao katika mkutano wa biashara na
uwekezaji katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya
Madola jijini London
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wadau mbalimbali wa biashara na
uchumi wa Uingereza aliokutana nao katika ukumbi wa Chatham House
jijini London