Askofu mkuu wa KKKT kanda ya dayosisi ya kaskazini Thomas Laizer akiwa anauombea mwili wa aliyekuwa muhasisi wa chama cha NCCR mageuzi katika ibada ya kumuombea iliyofanyika katika kanisa la OLigilai
viongozi wa NCCR mageuzi wakiwa mbele ya jeneza la marehemu Emanuel Petro Sirikwa muasisi wa chama hicho na mwanachama mwenye kadi namba tatu
Mwenyekiti wa chama cha NCCR mageuzi Jemsi Mbatia akitoa salam za chama
Vijana wa chama cha NCCR mageuzi wakiwa wamebeba jeneza la muhasisi wa chama hicho wakiongozwa na mtoto wa marehemu kuelekea makaburini
Mbunge wa viti maalum ambaye pia ni mbunge wa bunge la jumuiya ya Afrika mashariki kupitia tiketi ya chama cha NCCR mageuzi akiweka shada la maua
Askofu akiendesha misa ya mazishi makaburini
Alikuwa waziri mkuu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa na mke wake wakiweka shada la maua
Mke wa marehemu akiwa anaweka shada la maua katika kaburi la mume wake Emanuel Petro Sirikwa
Vyama vya siasa vimeaswa kuacha tabia ya kuchukiana na
kutoleana matamko ambayo hajajengi wala kusaidia jamii nabadala yake vyama
hivyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinabishana kwa hoja na maelezo ambayo
yanajitosheleza ili kuweza kuepusha migogoro mbalimbali ambayo inachangia sana kutokuwepo kwa amani
nchini
Kauli hiyo imetolewa na Askofu Thomas Laizer wa kanisa la
kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT)dayosisi
ya kaskazini kati wakati akiongea na
waombolezaji mbalimbali katika mazishi ya aliyekuwa muhasisi wa chama cha NCCR
Mageuzi Bw Emanuel Kisarika mapema jana Mjini hapa
Askofu huyo alisema kuwa kwa sasa asilimia kubwa sana ya viongozi wa vyama vya siasa wanatumia muda wao
mwingi sana kupambana na kutoa matamko ambayo
hayajengi taifa huku hali hiyo ikichangia kwa wingi sana kuwepo kwa mvurugiko wa amani ya nchi
Aliongeza kuwa endapo kama vyama vya siasa vingekuwa na
utaratibu wa kupendana wao kwa wao basi wangechangia kwa kiwango kikubwa sana hata wananchi wa Tanzania kuwa na Umoja lakini
baadhi ya vyama vimekuwa vikitumia vibaya nafasi zao za katika jamii hata
kuhasisha vitu ambavyo havifai kabisa
“leo vyama vinachukiana vinatoleana
maneno mabaya sana sasa haya maneno yanachangia kwa kiwango kikubwa sana
kuweza kuhatarisha hata amani ya nchi ni vema kama vikiacha hivyo na
hata kuangalia sasa changamoto
mbalimbali ambazo zinaikabili jamii husika:”aliongeza Askofu huyo
Pia alisema kuwa kama vyama hivyo vya siasa vitakuwa na
muonekano mzuri wa hoja basi vitaweza kupunguza hata matatizo mbalimbali ambayo
yapo kwenye jamii hasa tatizo la ukosefu wa umoja hasa kwenye matatizo ya
kijamii kama vile msiba kwa madai kuwa ni itikadi
za kisiasa
‘wapo watu wanaoelewa siasa kwa mtizamo wa tofauti sana
kwa baadhi yao sasa wanaacha hata
kusaidiana kutokana na itikadi za kivyama lakini kama siasa ya sasa itakuwa ni
siasa ya upendo basi itachangia kwa kiwango kikubwa sana kuweza kuwarudisha
hawa watu sehemu moja na kudumisha umoja ambao sasa unamezwa na uhaba wa
maarifa kutokana na mfumuko wa siasa ambao upo hapa nchini kwa sasa”aliongeza
Askofu Laizer
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi
hapa nchini Bw James Mbatia alisema kuwa watanzania wa leo wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanakuwa nan uzalendo wa kweli kama alivyo kuwa muhasisi wa chama
hicho Bw Emanuel Kasarika kwani uzalendo huo ni msingi mzuri sana wa kuweza
kuimarisha hata masuala mbalimbali hapa nchini
Bw Mbatia alisema kuwa endapo kama uzalendo wa vyama mbalimbali utaweza kudumishwa basi
wataweza hata kutatua matatizo mbalimbali ambayo yapo kwenye jamii kwa uraisi
sana tofauti na pale ambapo watu wanakosa uzalendo na vyama vyao pamoja na nchi
yao huku hali hiyo ikichangia sana umaskini ambao umekithiri sana.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia