Lema apinga Manispaa kuwahamisha Wamachinga mitaani

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbless Lema, amepinga Halmashauri
ya Manispaa Arusha, kuwahamisha mitaani wafanyabiashara ndogondogo
(Wamachinga) na amewataka warudi mjini kuendelea na biashara zao.
“Hatuwezi kuvumilia hilo, Wamachinga lazima wakae mjini, komaeni hapa
hapa,” alisema.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya uongozi wa Manispaa kuwaondoa
wafanyabiashara hao kwenye mitaa mbalimbali mjini hapa.
Alisema hayo juzi wakati akiwahutubia wakazi wa eneo la Kijenge
Mwanama, Kata ya Olorien, ambapo pia alifungua tawi la chama.
Baada ya kuondolewa mitaani, wamepelekwa eneo la wazi la NMC Ltd,
ambalo halina miundombinu yo yote, huku wengine wakiwa wamekosa maeneo
ya kufanyia biashara.
Hali hiyo iliwafanya mamia kwa maelfu ya wafanyabishara hao kuvamia
kiwanja kilichopo jirani na soko la Kilombero na kugawia maeneo kwa
ajili ya kufanya biashara.
“Tatizo la Wamachinga linahitaji muda mrefu kutatuliwa na sio siku
moja, “ alisema na kuongeza, “sasa hivi kumekuwepo na mgogoro kati ya
Manispaa na Wamachinga lakini chanzo ni Meya wa Manispaa ambaye
amepewa nafasi hiyo kwa bunduki.”
“Hatuwezi kuvumilia…Manispaa imeshindwa kuandaa miundombinu kuwafanya
Wamachinga waendelee na biashara zao bila kubugudha na badala yake
wanawafukuza kwa madai eti wanaleta uchafu, Wamachinga komaeni hapa
hapa mjini,” alisema.
Alisema kwa mfano, wamachinga wapelekwe kufanya biashara kwenye uwanja
wa mpira kwa sababu ulijengwa kwa nguvu za wananchi lakini uwanja huo
unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumzia kuhusu kazi ya ukombozi, Lema alisema ni ngumu na watu
wengi wanashindwa kutokana na usaliti.
Hata hivyo, katika kipindi hiki ambacho yupo kwenye ‘fungate’ (baada
ya mahakama kutengua ubunge wake) amepata muda  wa kutosha wa kuichapa
CCM sio kwa Arusha bali nchi nzima.
Alisema ataendelea kupigania haki za Watanzania jambo ambalo
atalifanya kwa nguvu zake zote bila kuogopa kwa sababu alizaliwa siku
moja na atakufa siku moja.
Aliwashambulia vigogo wa CCM ambao wameficha mabilioni ya fedha za
serikali katika benki za Uswisi, huku akisema anasikitishwa na
serikali kushindwa kuchukua hatua za haraka kuzirejesha fedha hizo na
kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia