WILAYA CCM ZAANZA UCHUZI LEO
UCHAGUZI wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani Chama Cha\ Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Arusaha, unaanza leo kwa wagombea wa nafasi za ngazi ya
wilaya na kwa ngazi ya mkoa atafanyika Oktoba 11.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa, Loota Sanare Mollel, ambaye
anatetea nafasi yake, alithibitisha kwamba uchaguzi kwa ngtazi ya
wilaya zote unafanyika leo na kwa mkoa ni Septemba 11.
Aliwataja wanaowania nafasi za uenyekiti wa mkoa kuwa ni Sheikh Adam
Ibrahim Chorah, Onesmo Koimerek Nangole na Dk. S\alash Mokosyo Toure.
Kwa upande wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa ni Isack Joseph
Copriano, Jasper Kishumbua na Loota Sanare wakati nafasi ya Katibu wa
Uchumi na Fedha mkoa ni Hilal Ramadhan Soud, Julius Mungure na Juma
Said Lossini.
Wanaogombea uenyekiti kwa Wilaya ya Arumeru ni Abraham Mathew Ole
Sella, Joel Alphayo Mollel na Nugu Raphael Long’idu Mollle na kwa
Wilaya ya Arusha ni Jubilate Shileitiwa Kiieo, Mussa Hamis Mkanga na
Wilfred Ole Soilel Mollel wakati Wilaya ya Karatu ni Gerald John
Gwava, John Zacharia Tippe na Mstapha Kassim Mbwambo.
Wagombea wa nafasi hiyo kwa Wilaya ya Longido ni ni Emmanuel Lukas
Laizer, Kishil Ole Nabak Mollel na Mokoro Saruni Laizer na kwa Wilaya
ya Meru ni Severena Richard Minja, Furahini Nderea Mungure na
Chrispher Richard Pallangyo, wakati Wilaya ya Monduli ni David Pello
Kivuyo, Reuben Ole Kunney na Olomon Kisika Lukunay na Wilaya ya
Ngorongoro ni Ibrahim Sumat na Metui Aile Ole Shaudo.
Wanaogombea nafasi za Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Wilaya
ya Arumeru ni Fanuel Loishsiye Kivuyo, na Mathias Erasto Manga, wakati
wagombea wa nafasi hiyo Wilaya ya Arusha ni Godfrey James Mwalusamba,
Harold Lyimo Adamson na Paulo Lotha Laizer, na Wilaya ya Longido ni
Michael Lekule Laizer, Parteyei Michael Syokino na Peter Reuben
Mushao.
Wagombea wengine katika Wilaya ya Karatu ni Abdul Ramadhani Barie,
Daniel Awack Tlemai na Daniel Tsingay Illakwahhi na katika Wilaya ya
Meru ni Elishilia Daniel Kaaya, Meja mtraafu Irikael Sifael Mbise, na
Julius Wilfred Mungure, wakati wagombea katika Wilaya ya Monduli ni
Edward Ngoyai Lowassa, Dk. Salash Mokosyo Toure na Nanai Taon Konina
na kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro ni Mathwe Ole Nasei, Abraham
Manase Mrase na Saning’o Ole Telele.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia