Wanachama waikaba koo TFA kwa kupata hasara, kukosa gawio

CHAMA cha Wakulima cha Tanganyika (TFA) kimelalamikiwa na wanachama
wake kwa kushindwa kutoa gawio kwa muda mrefu kwa kile kilichoelezwa
kuwa kimekuwa kikipata hasara kila mwaka.
Mkulima Raphael Charles Maro kutoka mkoani Kilimanjaro, alilalamika
kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa
wiki kuwa hajapata gawio kwa miaka 15 au 20 hivi.
Alishangaa kusoma taarifa kwama  chama hicho kimekuwa kikip;ata hasara
kila mwaka na akataka uongozi utoe maelezo ya kina, la sivyo wanaweza
kutoa azimio kwa mwaka mwingine.
Mkulima mwingine Ally Rashid Mwamba kutoka Kilimanjaro, alisema hakuna
hata mwaka mmoja kwa zaidi ya miaka 30 ambayo amepata gawio. Hata
hivyo alisema uongozi huo umekuwa ukiwapa bonsai ya kuongezea hisa.
Alihoji kwa nini TFA  iwe inapata hasara wakati ina vitega  uchumi vingi.
“Uongozi ni mbovu na tungependa ubadilike au watoke,” alisema.
Kwa upande wake, mwanachama Anna Jonas Mfinanga kutoka Dar es Salaam,
alilalamikia kutopewa gawio kila mwaka na badala yake wanaambiwa
kwamba inaingia kwenye thamani ya hisa.
Alishangaa na kusema hisa inaongezeka lakini hawapati gawio lo lote,
lakini hata hivyo, alionyesha matumaini yake kwamba iwapo uongozi huo
uliokaa madarakani kwa muda mrefu  utabadilikia kuna siku watapewa
gawio.
Alitaka katiba ya chama hicho ifanyiwe mabadiliko ili kuweka ukomo wa
nafasi ya uenyekiti ambayo imeshikiliwa na mtu mmoja kwa muda mrefu.
“Tatizo lipo kwenye uongozi, kwa mfano, mwenyekiti ni yule yule miaka
yote na hakuna mawazo mapya ya maendeleo,” alisema.
Mapema akisoma taarifa ya Mwenyekiti wa TFA, Elias Mshiu, kuhusu
matokeo ya biashara ya mwaka kwa ujumla, Katibu wa TFA, Wilson Malya
alisema jumla ya Sh. Bilioni 5.8 faida ghafi ya Sh. Milioni 576
ilipatikana.
Hata hivyo, alisema kiwango hicho ni pungufu kwa Sh. Milioni 150 au
asilimia 21 ikilinganishwa na kiasi cha  Sh. Milioni 725, faida ghafi
ya mwaka wa fedha auliopita.
“Mwaka huu wa fedha kumekuwa na anguko kubwa la faida ghafi kutoka
asilimia 14 katika mwaka wa 2010 hafi kufikia  asilimia 10 mwaka huu,”
alisema.
Alisema kupungua kwa faida ghafi kunatokana kwa kiasi kikubwa na
mfumuko wa bei, faida ndogo inayopatikana katika uuzaji wa mbolea na
mbegu bidhaa ambazo zimetawala mauzo yao.
Aidha alisema faida ndogo sana ilipatikana katika p;embejeo za kilimo
zilzouzwa kwenye mpango wa ruzuku kwa njia ya vocha.
“Baada ya kutoa gharama za uendeshaji za jumla ya Sh. Bilioni 2.0 na
gharama za kifedha za jumla ya Sh. Milioni 208, tumepata hasara ya Sh.
Milioni 390 ikilinganishwa na hasara ya Sh. Milioni 111 iliyopatikana
mwaka uliopita,” alisema.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia