TACAIDS yashauriwa kuongeza kasi dhidi ya maambukizi mapya
TUME ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), imeshauriwa kuongeza kasi
zaidi ya mapambano dhidi ya maambukizi mapya kwa kutoa elimu kwa
jamii ili wachukue hatua za kujiepusha na maambukizi yanayoathiri
nguvu kazi ya taifa.
Afisa Tawala Mkoa wa Arusha, Exaud Mwanga, alisema hayo alipokuwa
akifungua kikao cha siku moja cha viongozi wa madhehebu ya dini,
Mkoani Arusha kuhusu mwitikio na ushiriki wao, katika mapambano ya
ugonjwa wa Ukimwi, kilichoaandaliwa na TACAIDS.
Alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na madhehebu ya dini
kwa kushirikiana na TACIDS na wadau wengine kutoa ushauri wa kiroho
kwa watu waishio na Virusi Vya Ukimwi ambao unasaidia kuwafariji na
kuishi kwa matumaini.
Alisema mchango unaotolewa na madhehebu ya dini, katika kupunguza
ongezeko la maambukizi ya ukimwi, ni mkubwa, hivyo mchango huo bado
unahitajika zaidi ngazi za kata na vijiji, ili kupunguza ongezeko la
maambukizi mapya.
“Nasema hivi kwa sababu hali ya sasa kiwango cha maambukizi ni
asilimia 8.7 na vijini ni asilimia 4.7, hivyo tukiongeza juhudi zaidi
tutapunguza maambukizi haya,” alisema.
Awali Kamishina wa Tume ya Ukimwi nchini, Askofu mstaafu wa KKKT,
Peter Mwamasika , alisema taasisi za dini zina wajibu mkubwa wa
kutoa misaada ya kimalezi, kiafya, kielimu, kiushauri, kisheria kwa
waathirika ambao ni waumini wao, ili waepuke kupata maambukizi
mapya.
Alisema taasisi za dini lazima zitambue kuwa zina wajibu wa kuwatunza
yatima na wajane, wasiokuwa na uwezo, ambao wanatokana na vifo vya
ukimwi, ili kuwaanzishia miradi ya kiuchumi na kuachana na tabia ya
kuwaombea dua na kuwaacha waende zao bila kuwawezesha.
Aliwaambia viongozi hao kuwa TACAIDS ina jukumu kubwa la kuhamasisha
watu, waeleze mahitaji yao kuhusu mapambano dhidi ya ukimwi,
kuwaepushia kupata maambukizi mapya na kupitia Tacaids, serikali
inazifikia taasisi za dini, ili ziweze kusaidia kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu madhara ya ukimwi na hatua za kuchukua kwa ajili ya
kujikinga na maambukizi mapya.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia