Mlima uliokuwa wa kwanza barani africa kwa urefu kuliko milima yote africa.


Mlima uliokuwa wa kwanza barani africa kwa urefu kuliko milima yote africa sasa watanzani kazi kwetu kupigia vivutio vyetu kura

Kama haujawahi kutembelea nchi ya tanzania au katika vivutio vya utalii ikiwemo mlima kilimanjaro fanya hiuma kufanya hivyo kwa sababu kuna vitu vingi na vizuri vya kujifunza kuhusu mlima Kilimanjaro na pia katika hifadhi yake iliyopo Kilimanjaro kama unavyoona katika picha iliyopo hapo chini. Mlima huu unahistoria ndefu sana kwanzia mwanzo wake mpaka sasa.karibu katika mlima na kuweza kuupanda na kufika kileleni na kuona theluji iliyoko juu ya mlima huo. Wengi waliopanda wamejionea kwa macho yao bado wewe nawe nakusihi ukajionee kwa macho yako mlima huu.karibu Tanzania,karibu hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro. Na pia katika bara hili la africa katika nchi ya tanzania kuna mbuga za wanyama kama vile serengeti , ngorongoro conservation , manyara , selous na pia zipo ndogondogo katika pwan kusini na tanzania lakini watu wote mnaotaka kufika katika mbuga hizo lazima mpitie katika lango kuu la kiwanja cha ndege cha mwalimu nyerere au kiwanja cha ndege cha kilimanjaro international air port .bei au viingilio vya vivutio vya nchi yetu ni rahisi na kila mtu anakaribishwa kuingia bila woga wowote.

Kilimanjaro Mlima mrefu kuliko yote Africa

kibo na mawenziKaribu Tanzania kuona mlima mrefu kuliko yote africa.Historia fupi kuhusu mlima Kilimanjaro,mlima huu ulikuwa ni wa volcano na sasa ni mlima tulivu wa volcano nikimaanisha kuwa volcano yake imetulia na haitoki tena.mlima huu una urefu wa mita 5895.Uko katika mkoa wa Kilimanjaro nchini tanzania mpakani na kenya.Mlima huu unavilele viwili ambavyo ni kibo na mawenzi.Vilele hivyo vilitenganishwa na volcano hiyo.

Mlima huu ni wa volcano na umetulia volcano yake kwa muda mrefu sasa.Pia mlima huu unatheluji nyeupe inayongaa kama jua linavyongaa.kupanda mlima huu kunategemea na njia gani uliyopitia kuna njia kama nne za kupandia,mmoja ni marangu , pili ni moshi mjini na nyinginezo nyingi.picha iliyoko hapo chini inaonyesha vilele hivyo ambavyo ni kibo na mawenzi.kama unatakakufika africa unatakiwa kufika kwanza tanzania ambapo ni katika mji wa dar es salaam.

About woinde

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia