Shirika la
hifadhi za taifa (TANAPA)wamewataka watanzania kuipigia kura vivutio vya asili
barani Afrika ikiwemo Mlima Kilimanjaro,Bonde la hifadhi za Ngorongoro,na Mbuga
ya Serengeti iliviweze kuingia kwenye shindano la kutafuta maajabu saba ya
asili ulimwenguni.
Akizungumza
na libeneke la kaskazini Meneja mahusiano wa shirika hilo Pascal Shelutete alisema kuwa Tanzania
imebahatika kuingiza vivutio hivyo na kuwataka Watanzania kuipigia kura vivutio
hivyo kwani Serengeti imeweza kingizwa kwa sababu ya kuhama kwa wanyama aina ya nyumbu,kwani ni tukio adimu hapa
ulimwenguni.
Alisema kuwa
wapiga kura wanatakiwa kuchagua vivutio hivyo na kuvipigia kura iliviweze
kupita na pia unatakiwa kuongeza vivutio vingine 4 unavyovifahamu ilikuweza
kupata vivutio saba vilivyopo barani Afrika na kuuelezea mlima Kilimanjaro upo
kwenye mstari wa tropiki na ni joto lakini unatheluji ambayo haikauki kwa
majira yote.
Shelutete
alisema kuwa utaratibu wa kupiga kura unatumika kwa kutumia barua pepe na kuwa
wao kama tanapa wanashirikiana na wadau mbali mbali nkuweza kuona kuwa Tanzania
inaingizwa kwenye moja ya maajabu hayo saba.
Aidha alisema
kuwa mbali na kuwataka kupiga kura pia wanaendelea kuwahamasisha watanzania
wakishirikiana na wadau mbali mbali ilikuweza kuwafahamisha watapata faida gani
watanzania ilikuweza kuwahamasisha wale wote waliotembelea kwenye mbuga wakiwa
ni wageni na watanzania kuweza kupigia kura vivutio hivyo.
Shelutete
Faida tunayoipata ni kuendele kuvitangaza vivutio hivyo kwenye mataifa mbali
mbali hivyo tutaweza kuongeza wageni watakaokuja kutembelea vivutio hivyo na
kuongeza pato la uchumi na la taifa hadi sasa waratibu wa shindano hili hawajatoa
nani yupo kwenye nafasi ipi lakini tunaimani kuwa hadi ifikapo mwezi wa December
ambapo shindani hilo litafikia tamati ya upigaji kura tunaimani nasi tutakuwa
ni mojawapo ya maajabu hayo ya afrika.
Shelutete
alisema kuwa Shindano la kuchagua maajabu saba ya Afrika limeandaliwa na
shirika la Seven Natural Wonders lenye makao yake makuu Texsas Nchini marekani
na madhumuni ya shindano hili ni kutafuta maajabu saba ya Ulimwengu na kutoa
sifa ya mbuga ya Serengeti ambapo kwa miezi 12 wanyama wanahama kutoka eneo
moja kwenda nchi kufuta malisho.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia