KATIKA kile
kinachoonekana ni kujiimarisha kuelekea
uchaguzi mkuu wa urais mwaka 2015 kambi inayohusishwa na waziri
mkuu mstaafu aliyejizulu,Edward
Lowasa imeibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa CCM wilaya ya Arusha mjini.
Katika
uchaguzi huo uliokuwa na kila aina ya vituko mwenyekiti wa zamani wa CCM wilaya
ya Arusha,Jubilate Kileo aliangushwa vibaya na mpinzani wake,Dk Wilfred Ole
Soilel ambaye ni daktari wa hospitali ya
St,Elizabeth kwa tofauti ya kura 70 .
Kinyanganyiro
kingine kilikuwa kwenye nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa(Nec)
ambapo,Godrey Mwalusamba ambaye ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya alifanikiwa
kupata kura 449 na kuwaangusha vibaya wapinzani wake ambao ni ,Loota Laiser
aliyepata kura 79 na Dk Harold Adamson aliyeambulia kura 7.
Kitendo cha
wajumbe wa mkutano mkuu kumchagua Dk Ole Soilel anayehusishwa na kambi la
Lowasa kuliibua simanzi kwa kambi nyingine ambapo katika hali isiyo ya kawaida
mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo sanjari na katibu wa CCM Arusha,Mary
Chatanda juzi walionekana kuwa wanyonge muda wote kitendo kilichoibua maswali
mengi kwa baadhi ya wajumbe
waliohudhuria uchaguzi huo.
Katika hali
isiyo ya kawaida Kileo pamoja na wafuasi wake walikacha kabla ya kutangazwa kwa
matokeo ya uchaguzi huo lakini alipotafutwa na gazeti hili kwa njia ya simu
alikataa kuweka wazi endapo ameridhika na matokeo ya uchaguzi huo na kudai
kwamba kilichofanyika ni kuondoa kundi moja na kuingiza kundi lingine.
Hatahivyo,kijana mmoja ambaye ametajwa kuwa ni
mfuasi wa kundi la Kileo alipewa kichapo nje ya ukumbi wa uchaguzi ndani ya
hoteli ya Naura jijini hapa kwa kile kinachodaiwa ni kutoa lugha chafu kwa wafuasi wa Musa Mkanga ambaye naye alikuwa
akiwania nafasi ya uenyekiti wa CCM wilaya.
Awali kabla
ya uchaguzi huo taarifa zilizolifikia LIBENEKE LA KASKAZINI zimedai ya kwamba ndani ya
ukumbi wa uchaguzi Kileo aliulizwa maswali na wajumbe wa mkutano huo kwamba
aeleze sababu za yeye kushindwa kusimamia jimbo la Arusha mjini lililoangukia
upinzani pamoja na kata yake ya Kaloleni hali iliyompa wakati mgumu kujibu
maswali hayo.
Hatahivyo,taarifa
zilizowakariri baadhi ya wajumbe ndani ya mkutano huo zimedai kwamba Kileo
nusura aangue kilio ambapo alikaririwa akiwaambia wajumbe ya kwamba wamhurumie
kwa kuwa yeye ni mzee na endapo akichukia itakuwa laana kwao.
“Kileo
alipigwa swali kwamba yeye kama mwenyekiti wa wilaya kwanini hakusimamia jimbo
hadi likaangukia upinzani lakini pamoja na kata yake ya Kaloleni ndipo akajibu
kwamba yeye ni mzee wamhurumie kwani akichukia huenda akawaachia laana”kilisema
chanzo cha habari ndani ya mkutano huo
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo,katibu wa CCM wilaya ya Longido,Esupat Naikaya
alitangaza nafasi ya uenyekiti wa wilaya na kusema kwamba kura halali
zilizopigwa ni 538 ambapo wagombea Musa Mkanga alipata kura 1,Jubilate Kileo
alipata kura 232 na Dk,Wilfred Ole Soilel alipata kura 305 na kutangazwa
mshindi.
Wengine
waliotangazwa ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kuwa ni mkuu wa mkoa wa
Arusha,Magesa Mulongo,Halima Mamuya,Fatuma Ngairo,Musa Mkanga pamoja na Getrude
Haule.
Kwa upande
wa wajumbe wawakilishi wa mkutano mkuu wa CCM mkoa waliotangazwa washindi ni
Agrey Mushi pamoja na Gasper Kishumbua .
Awali akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi
mwenyekiti mteule wa CCM wilaya,Dk Ole Soilel aliwashukuru wajumbe waliompatia
kura na kuwaambia kwamba wana kibarua kikubwa cha kuhakikisha wanapambana na
upinzani uliojiimarisha wilayani Arusha.
“Tuna
kibarua kikubwa cha kupambana na upinzani hapa Arusha nyine ni mashahidi hapa
mjini bendera za wapinzani zimeenea kila kona za kwetu hakuna kama kwamba CCM
sio chama tawala”alisema Ole Soilel
Naye,Mwalusamba
pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha,Mulongo waliwashukuru wajumbe waliowapatia
kura katika uchaguzi huo huku wakihaidi kuwatumikia katika uongozi uliotukuka.
kwa
upande wa wilaya ya simanjiro Mbunge wa jimbo la Simanjiro Christopher
ole sendeka ameweza kupeta mara baada yakumshinda mpinzani wake Justine
Nyari kwa kura345 ambapo wapinzani wengine ambao ni lenganasa pamoja na
Awazo Omary walijito.
Katika
kura hizo jumla ya wapiga kura 610 walishiriki na sendeka aliweza
kupata kura 471 huku nyari akipata kura 126 kwa upande wa wenyekiti wa
wilaya Broun Methius ole suye aliweza kupata kura 423 na kunyakuwa
nafasi hiyo huku lengai Ole Makooo akipata kura
198.
mara
baada ya sendeka kutangazwa mshindi aliwashukuru wananchi wa wilaya
hiyo nakubainisha kuwa ata endelea kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo
kwa hali namali.
kwa
upande wa wilaya ya Babati vijijini nafasi ya mwenyekiti imechukuliwa
na Alhaji Songora ambaye amepata kura 656 ambapo mpinzani wake Laurenti
Fisso akipataa kura 264 na upande wa NEC Amani Hilji alipeta kwakupata
kura 531 na mpinzani wake Willy Bayo akipata kura 362 huku nafasi wa
tatu Peter Naali akipata kura 84 .
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia