MALULA SEKONDARI WALIA NA KERO YA MAJI
UONGOZI wa shule ya sekondari ya Malula iliyopo
King”ori wilayani Arumeru Mashariki mkoani Arusha umeiangukia serikali na
kuiomba itatue tatizo la kero ya maji inayowakabili shuleni hapo kwa madai
kwamba linachangia kudumaza kiwango cha elimu shuleni hapo.
Hatahivyo,uongozi huo umesisitiza ya kwamba
wanafunzi wa shule hiyo wanalazimika kutembea umbali mrefu kusaka huduma hiyo
na kujikuta wakipoteza muda mwingi wa masomo.
Akizungumza katika mahafali ya kwanza shuleni
hapo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mkuu wa shule hiyo,Rehema Mroso alisema kwamba shule yake imekuwa
ikikabiliwa na tatizo kuu la uhaba wa maji tangu ianzishwe huku akiiomba
serikali iwajengee matanki ya kuhifadhi maji kuokoa tatizo hilo.
Mroso,alisema kwamba baadhi ya wanafunzi wa shule
hiyo wanalazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kolomita 5 kusaka maji
kitendo ambacho kimechangia kudumaza kiwango chao cha elimu kwa kuwa wanatumia
muda mwingi kusaka maji.
Alisema kwamba tatizo la uhabaw a maji limechangia kuharibu
mazingira shuleni hapo kwa kuwa hukosa maji ya kuboreshea mazingira sanjari na
kusafishia vyoo mbalimbali shuleni hapo.
“Tuna tatizo kubwa la maji hapa shuleni kwetu
wanafunzi hutembea hadi Kia kusaka maji na kujikutab wanatumia muda mwingi
kuyasaka maji na kisha kupoteza muda wa masomo’alisema Mroso
Hatahivyo,alisisitiza kwamba wamekuwa wakibaliwa na
kero za uhaba wa jengo la utawala,maabara,uhaba wa nyumba za walimu sanjari na
tatizo la uzio wa shule hali ambayo inahatarisha usalama wa wanafunzi hususani
wa kike wanaolala shuleni hapo.
Awali akizungumza katika mahafali hayo mgeni ramsi
ambaye alikuwan ni katubu tawala wa mkoa wa Arusha,Exauds Mwanga alisema kwamba
serikali imepokea na italifanyia
kazi tatizo la kero ya maji lakini
aliwashauri kupanda miti ya kutosha kwa lengo la kuhifadhi mazingira shuleni hapo.
Mwanga,alikemea tabia ya baadhi ya wanfunzi hususani
wa kiume shuleni hapo kuvaa suruali zao chini ya makalio maarufu kama “mlegezo” huku akisisitiza ya kwamba uvaaji
huo ni marufuku hapa nchini.
Hatahivyo,alisisitiza kwa ukali kwamba serikali
itawachukulia hatua kali wale watakaobainika kununua mitihani ya kidato cha nne
na kudai kwamba wazazi wa wanafunzi watakaowasaidia watoto wao kununua mtihani
hiyo nao watakiona cha moto.
“Nimesema kwamba endapo mwaka huu Yule
atakayebainika kununua mtihani iwe mwalimu,mwanafunzi ama mzazi nitakufa naye
narudia tena nitakufa naye”alisema Mwanga
Aliwataka wazazi wa wanafunzi hao kuwaandaa watoto
wao kwa ajili ya mitihani ya kidato cha
nne na sio kuwapatia fedha za kununulia mitihani hiyo.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia