Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo (kulia) akipeana mkono na Askofu Gervas John Nyaisonga.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akibusu Pete ya Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisalimiana na Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Askofu mstaafu wa jimbo la Domama Mhashamu Baba Askofu Mathias Isuja.
Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga.
Kiongozi
wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo akiwa
na Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga wakifuatilia vikundi vya
kwaya vikitoa burudani.
Waumini
na watawa wakiwa katika foeni ya kwenda kumpa mkono wa kila la kheri
aliyekuwa Askofu wa jimbo lao ambaye amehamishiwa kitume jimbo la Mpanda
Mkoani Rukwa.
Kinamama wakatoliki wakiwa wamebeba zawadi ya mashine ya kufulia nguo na
Mashine ya kupoozea maji ya kunywa wakati wakielekea kumuaga Mhashamu
babab Askofu Gervas Nyaisonga.
Mamia
ya wakotiliki wamejitokeza kumuaga Askofu wa jimbo la katoliki
Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga ambaye anahamia Mpanda
kwa ajili ya kuendelea na kazi Dini.Sherehe hiyo iliyotanguliwa na
Ibada ilifanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mkoani
Dodoma.
Mgeni
rasmi katika sherehe hiyo ambayo alikuwepo Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu
Pina,alikuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini,Mwadhama Polcarp
Kardinal Pengo. Pia sherere hiyo ilihudhuriwa na Askofu mstaafu wa jimbo
la Domama Mhashamu Baba Askofu Mathias Isuja.
Katika
sherehe hiyo ,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga. alizawadiwa
vitu mbali mbali zikiwemo fedha taslimu.
Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga anaondoka rasmi Dodoma
kuelekea Mpanda Ijumaa tarehe 2 akipitia Tabora. Amehamishiwa kwa kazi
za Kichungaji Jimbo la Mpanda.
Pamoja
na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mama Rehema Nchimbi,Papadri na
watawa wote wa jimbo la Dodoma kulikuwepo vikundi vya kwaya kutoka
makanisa mbalimbali ikiwemo kwaya ya Kanisa analosali Mhe.Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, Kwaya ya Shirikisho Hananasifu Dar es Salaam.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia