Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Chalinze.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari
Chalinze, ambapo pamoja na kuwaambia tathmini ya CCM lakini aliwaambia
kuhusu namna ambavyo vyama vingine havijakuwa kidemokrasia kiasi cha
kuanza kubaguana hadi kwenye kampeni.
Mgombea wa CHADEMA Mathayo Torongey anayedaiwa kutelekezwa.
- Wabunge wagoma kuchangia kampeni Chalinze
- Washindwa kupeleka helkopta Chalinze
- Yadaiwa kisa ni ubaguzi walionao
Na Mwandishi Wetu,Chalinze
Torengei
ametelekezwa na Chadema kwasababu ya kabila lake na ukanda wake na ndio
maana hata helkopta wameshindwa kuipeleka ili kumsaidia kwenye kampeni.
Hayo
yalisemwa jana na Katibu na Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye wakati
akitoa tathimini ya hali ya kampeni za uchaguzi jimbo la Chalinze.
Alisema
kuwa viongozi wa Chadema wameonesha wazi kuwa hawana nia ya kumsaidia
Torengei na sababu kubwa ni moja tu kuwa si mwenzao.
"
Wabunge wa Chadema wamekuwa na utamaduni wa kuchanga fedha zinapotokea
chaguzi lakini kwa huyu mgombea wao wa Chalinze wamegoma kufanya hivyo.
"Wamekuwa wakifanya ubaguzi lakini sasa ni dhahiri kuwa wameonesha kile ambacho kipo moyoni mwao.
"Ukifanya
uchunguzi utabaini hakuna mahali ambapo Chadema hawakutumia helkopta
katika uchaguzi mdogo ambapo walishawahi kutumia helikopta kwa uchaguzi
wa Udiwani tu Arusha.
Alifafanua kuwa Torongei ametapeliwa na Chadema na hilo litakuwa fundisho kubwa kwake na kwamba ameingizwa mkenge.
"Anachotakiwa
kujua jamaa hao ni matapeli na ameingizwa mkenge.Tunajua baada ya
uchaguzi huu si atashindwa kupata kura bali atakuwa amefilisika,"alisema
Nape.
Aliongeza
kutokana na kumsusia uchaguzi huo, hata vijana ambao wameletwa na
Chadema kwa ajili ya kufanya vurugu wanaishi maisha ya kuomba omba.
"Wamewaleta vijana lakini nao wanaishi maisha ya kubahatisha.Wamefikia mahali vijana wao wanakuja kuomba fedha ya kula tunawapa.
"Hivyo
kama wao nao wameishiwa wasione aibu maana kitendo cha kumsusa mgombea
wao, wachache waliopo wanaishi maisha magumu sana,"alisema Nape.
Akizungumzia ushindi wa chama hicho, Nape alisema kwa hali ilivyo watashinda kwa zaidi ya asilimia 94.
"Ushindi
wetu katika uchaguzi unaotarajia kufanyika Aprili 6 ambayo itakuwa
Jumapili ni zaidi ya asilimia hizo.Wapinzani hawana lolote na
watashindwa vibaya kuliko wanavyotarajia,"alisema.
Kuhusu
kampeni zinazoendelea, alisema zinakwenda vizuri lakini wapinzani hasa
Chadema wanafanya hujma za kuiba shahada za kupigia kura kupitia watoto
ambao wanawapa fedha ili waziibe kwa wazazi.