Mkurugenzi
wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki akifungua rasmi
mafunzo ya stadi za uchunguzi yanayofanyika katika hoteli ya Naura
Spring jijini Arusha. Mafunzo hayo ya wiki moja kuanzia Machi 31—4, 2014
yamelenga kuwaongezea maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora (THBUB) stadi za kiuchunguzi hasa wanapofanya uchunguzi unaohusiana
na kazi za kila siku za Polisi. kushoto ni muwezeshaji kutoka Tume ya
Haki za Binadamu ya Afrika Kusini Bibi. Lindiwe Khumalo na kulia ni
Muwezeshaji Mkuu wa mafunzo hayo Bwana Sean Tait kutoka African Policing
Civilian Oversight Forum (APCOF).Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika
la GIZ.
Sehemu
ya washiriki wakiwa katika Mafunzo, wa kwanza kushoto ni Afisa
Uchunguzi wa THBUB, Bwana Godian Binamungu na kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Msaada wa Sheria, Bwana Nabor Assey na anayeonekana kwa mbali
ni Afisa Uchunguzi , Bi. Nancy Ngula.
Maafisa
wa THBUB wakimsikiliza kwa makini Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait
(hayupo pichani).Kutoka kushoto ni Bibi Monica Marealle (katikati) ni
Bwana Elias Sowani na (kulia) ni Bwana Pontian Kitorobombo.
Muwezeshaji
Mkuu, Bwana Sean Tait akiongea na Maafisa wa THBUB wanaoshiriki
mafunzo(hawapo pichani) na kuwataka kuwa wasikivu ili kwa pamoja waweze
kupata faida kutokana na mafunzo hayo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya
Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki.
Maafisa
Uchunguzi wa THBUB wakijifunza kwa vitendo namna ya kukabiliana na
Matukio yanayohusiana na uvunjwaji wa haki za binadamu.
Muwezeshaji
wa Mafunzo kutoka THBUB, Bibi Jamila Sulu akiwapa maswali ya “chemsha
bongo” Maafisa wa THBUB kwa lengo la kupima kumbukumbu ya kile
walichojifunza.
Muwezeshaji
kutoka African Policing Civilian Oversight Forum (APCOF) akiwasilisha
mada inayohusu Uandaaji wa ushahidi Mahakamani.
Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait akiwasilisha Mada ya kwanza inayohusu Haki za binadamu na masuala ya Polisi.
Maafisa wa THBUB wakijadiliana katika kazi za vikundi ambazo ni sehemu ya Mafunzo hayo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala Bora, Hajat Fatuma Muya akichangia jambo katika
mafunzo hayo.Anayemsikiliza ni Afisa Uchunguzi, Bi. Farida Ndege.
Maafisa
Uchunguzi wa THBUB wakifanya mafunzo kwa vitendo kutoka ( Kushoto) ni
Bi. Vivian Method na (kulia) ni Bi. Makihiyo Mrutu.
Sehemu ya washiriki wakipitia makabrasha wakati mafunzo hayo yakiendelea.
Muwezeshaji
kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini Bibi Lindiwe Khumalo
akichangia jambo katika mafunzo hayo, kulia ni Muwezeshaji Bi. Louise
Edwards.
Maafisa Uchunguzi wa THBUB katika kazi za vikundi wakati wa mafunzo.
Bwana
Mokgapi Maleka , Afisa kutoka shirika la GIZ la Afrika Kusini ambalo
ndio wafadhili wakuu wa Mafunzo hayo akiongea na washiriki.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji.