KAGERA SUGAR WAKOMALIWA NDANI YA UWANJA WA NYUMBANI


Timu zikisalimianaTimu zikipanga mstari mmoja tayari kusalimiwa na mgeni rasmi na viongozi mbalimbali
Afisa utamaduni Mzee Rugeiyamu akisalimiana na Marefa na timu kiujumla


Kocha mkuu wa JKT Ruvu

Lineup ya Wachezaji wa Kagera Sukari
Timu zikisalimiana.
Marefa wa Mechi hii

Timu ya JKT Ruvu ikiomba kabla ya mtanange kuanza
 Timu ya Kagera Sugar ikiomba nayo


Makapteni wakisalimiana na marefa 
Kocha wa Kagera Sugar akicheka kwa furaha mara baada ya kuongea nae
picha ya pamoja.
 Kagera Sugar jioni hii wamelazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu ya Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sare hiyo imeisaidia JKT kupanda kwa nafasi moja kutoka ya 13 hadi ya 12, juu ya JKT Mgambo ya Tanga, wakati Kagera imelingana kila kitu sasa na Yanga, pointi na wastani wa mabao, zikiwa katika nafasi ya nne na ya tano.
Sare hii, maana yake Kagera imeshindwa kuendeleza wimbi la ushindi waliloanza nalo juzi, wakiifunga Yanga 1-0, kwa bao pekee la Themi Felix katika dakika ya 67 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Felix aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.
Ligi hiyo, itaendelea kesho kwa mchezo mmoja, utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baina ya wenyeji Toto African na Yanga SC.
 

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia