Mkurugenzi
wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga kulia akizungumza na
waandishi wa habari juu ya kuanza kuuzwa kwa tiketi za shindano la Taifa
la Redds Miss Tz kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tz
Bosco majaliwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya
LINO AGENCY Hashim Lundenga amesema kuwa,Kutokana na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila tiketi itagarimu kiasi cha shilingi laki moja (100,000) za kitanzania.
Kwa upande wa burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii nguli hapa nchini kama Diamond Platnum,Winfrida Josephat’Rachel’s pamoja na Wanne star ngoma troupe.