CRISTIANO RONALDO ANUNUA GARI MPYA YENYE THAMANI YA SH. MILIONI 415, LINA UWEZO WA KUCHANGANYA MWENDO WA HADI KILOMITA 100 KWA SAA
MADRID, Hispania
NYOTA wa Real Madrid,
Cristiano Ronaldo amejawa na furaha tele kutokana na kiwango cha juu
alichoanza nacho msimu huu na kuamua kujipongeza kwa kujinunulia gari
dogo jipya la kifahari kwa ajili ya kutanulia mitaani.
Gazeti la Marca limeandika leo kuwa Ronaldo amenunua gari hilo jipya aina ya McLaren MP4-12C Spyder kwa dola za Marekani 268,000 (Sh. milioni 415).
Gazeti la Marca limeandika leo kuwa Ronaldo amenunua gari hilo jipya aina ya McLaren MP4-12C Spyder kwa dola za Marekani 268,000 (Sh. milioni 415).
Sifa
mojawapo kubwa ya gari hilo la kisasa ni kasi yake ya kuchanganya
mwendo kwani linapowashwa tu, huwa na uwezo wa kufikia spidi ya kilomita
100 kwa saa baada ya muda mfupi wa sekunde 3.1.
Ronaldo alionekana juzi katika maeneo ya kwao, Lisbon nchini Ureno ambako amekwenda kuungana na wenzake katika kambi ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno.
Mbali na gari hilo jipya (McLaren MP4-12C Spyder) Ronaldo pia anamiliki magari kadhaa ya kifahari likiwamo aina ya Lamborghini Aventador LP700-4.

Dude jipya alilonunua Ronaldo, McLaren MP4-12C Spyder
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia