JUMLA YA SHILINGI MIL.48ZIMEPATIKANA KATIKA HARAMBEE YA SHULE YA SEKONDARI PEACE HOUSE



Jumla ya shilingi milioni 48 zimepatikana katika harambee ya kuchangia shule ya watoto yatima ya Peace House iliyopo Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha inayomilikiwa na kanisa la kiinjikli la kilutheri Tanzania.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo iliyoambatana na mahafali ya pili ya kidato cha nne mgeni rasmi Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kati  Dkt. Thomas Laizer  amesema kuwa watoto yatima ni sehemu ya jamii hivyo ni vyema kama jamii itabadili mtizamo yao na kuwapatia haki sawa iliwaweze kufikia malengo yao kama ilivyo kwa watoto wengine.

Dkt.Laizer amesema kuwa jamii imekuwa ikiwatenga watoto yatima haswa ndugu wa yatima hao hali ambayo inapelekea kukosa mahitaji ya msingi kama elimu.
Aidha amesema kuwa watoto yatima wanahitaji mahitaji  muhimu kama walivyo watoto wengine na pindi wanapopata nafasi ya kujiendeleza kielimu daima huwa wananfanya vizuri.

Pia amewahimiza watanzania kuendelea kuwasaidia yatima bila kusubiri wafadhili kutoka nje kwa kuwa vitabu vitakatifu vya dini vinahimiza kuwasaidia watoto hawa ambao wengi wao wamejaa sononeko la kuondokewa na wazazi wao.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Christopher Augustine Mushi amemshukuru baba Askofu na wadau wote waliochangia harambee hiyo kwa kuwa wamesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili kwa sasa ambapo itakumbukwa kuwa wafadhili wa shule hiyo walijitioa kufadhili.

Mushi amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na hapo awali ilikuwa inafadhili asilimia mia moja kwa miaka mine mfululizo  na ilikuwa ikichukua watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Lakini mwaka 2011 taswira ya wafadhili ilibadilika gafla ambapo walitaka kufunga shule hiyo kwa miezi 18 tangu September hadi  march 2013 hali ambayo ilitoa tasiri mbaya na isiyokubalika katika sera ya elimu sheria za nchi na jambo hili lilipigwa na bodi vikali  pamoja na dayosisi katika vikao vyao mbali vilivyofanyika .

Pia mkuu huyo aliongeza kuwa shule hiyo ni jumba la kuandaa viongozi wazalendo na wenye uchu nan nchi yao hasa katika kazi ya usimamizi wa rasilimali ya za nchi.
Amesema kuwa msingi imara wa taifa la leo ni kuwajengea watoto elimu ya kujitengemea ili pindi ambapo wanapohitimu elimu yao ya vyuo vikuu kutotegea kuajiriwa bali wafikirie kuajiriwa zaidi.

Shule ya Peace House kwa sasa ina jumla ya wananfunzi 344 ambapo wanafunzi 61 walihitimu elimu ya kidato cha nne ambapo shule hiyo kwa sasa ni mcghanganyiko kwa wanafunzi ambao ni  yatima na wanaolipiwa karo na wazazi wao.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia