MGOMBEA UDIWANI(CHADEMA)ASHIKILIWA NA POLISI ARUSHA

Mgombea udiwani akiwa anapanda gari la polisi

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mgombea Udiwani katika kata ya Daraja mbili mkoani Arusha   Prosper  Msofe anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa makosa ya kumshambulia Bw Rama Kalamba ambaye ni Mhamasishaji mkuu wa kampeni za kusafisha jiji  hasa kwa wafanyabaishara wadogo wadogo “Machinga”

Akiongea na libeneke la kaskazini, mjini hapa kamanda wa Polisi bw Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana  majira ya saa mbili na nusu katika eneo la france Kona ambapo mtuhumiwa huyo alimshambulia mhamasishaji wa Jiji la Arusha  na kusababisha madhara makubwa

Kamanda Sabas aliongeza kuwa ndani ya eneo hilo mgombea huyo alikuta mhasishaji wa Jiji akiwa katika shuguli zake za kawaida ambapo alikuwa anawatoa wanawake ambao walikuwa wanauza bidhaa nje  ya soko la muda la viwanja vya Nmc  na ndipo mgombea huyo alipohoji uhalali wa kuwatoa wanawake hao katika eneo hilo

Alisema kuwa mara baada ya kumuhoji mhasishaji huyo mtuhumiwa huyo alimfanyia shambulio kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake hali ambayo ilisababisha Tafrani kubwa sana katika eneo hilo ambalo wafanyabaishara walikuwa wanaendelea na biashara zao

‘baada ya kuhoji alivunja sheria na kuanza kumsambulia kwa kumpiga haraka haraka huyu mhasishaji ambaye yupo kwa mujibu wa sheria ya Jiji bila kujua kuwa anavunja sheria ya Nchi na ndipo tulipopata taarifa juu ya tukio hilo na kisha kufika na kumchukua mtuhumiwa huyo ambaye alikatiwa RB namba AR/RB/12648/2012 ambapo kosa ni shambulio la kawaida katika kituo cha polisi cha Kati”alisema

Awali katibu wa Chadema kwa Wilaya ya Arusha  Martin Sarungi alisema kuwa pamoja na kuwa polisi walimshikilia Mgombea huyo lakini bado wamefanya uonevu wa hali ya juu sana na hiyo ni  mipango ya kumuondoa katika uchaguzi wa kata ya daraja mbili.

Aliongeza mahali ambapo wanapoona kuwa ni uonevu ni pale ambapo polisi walimpeleka katika zahanati ya Polisi kwa ajili ya kutibiwa majeraha mbalimbali ambayo walikuwa nayo lakini askari hao waliokuwa na silaha kali za moto walimpeleka moja kwa moja hadi mahakama ya Maromboso ambapo pia mshatakiwa wao hakuweza kusomewa mashitaka kutokana na kuwa na hali mbaya ya kiafya hali ambayo iliwalazimu kumrudisha katika Hospitali ya Mount Meru

“sasa hapa unaona hawa polisi wanashirikiana na chama tawala na hizi ni mbinu tu ila hata wafanyeje sisi bado ile ni kata yetu kwa sababu wewe huwezi kumchukua mtu useme kuwa unampeleka zahanati kumbe unampeleka mahakamani ukifika mahakamani chini ya ulinzi mkali unashindwa kusoma mashitaka kutokana na kuzidiwa  na kipigo unamchukua tena na kisha kumrudisha hospitali ya mkoa chini ya uangalizi wa polisi je tueleweje kama sio mbinu za kisia

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia