
Kampeni
za CHADEMA kuwania kiti cha Udiwani katika kata ya Daraja Mbili mkoani
Arusha zilizinduliwa Jumamosi Oktoba 6 2012, huku Sakata la hivi
karibuni la kutoroka kwa mahabusu chini ya ulinzi mkali wa askari polisi
katika mahakama kuu ya kanda ya Arusha likichukuwa sura mpya na
kutawala kampeni hizo.
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki Kamanda mpambanaji Joshua Nassari maarufu
kama (Dogo janja) akifungua kampeni hizo alionyeshwa kushangazwa kwa
hatua hiyo huku akidai kuwa Serikali isipo chukua hatua dhidi ya
watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti (CHADEMA) Usa River basi ni
wazi kuwa patachimbika na Nchi haitatawalika wala kukalika
akishangiliwa
na umati mkubwa uliohudhuria uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa
udiwani katika kata ya daraja mbili alidai kuwa ni maigizo tu hayo
yanayoendelea na CHADEMA hawapo tayari kuchezewa filamu hiyo kamwe

Kamanda Lema akihutubia umati mkubwa wa watu
Habari
za ndani zinasema kuwa mahabusu hao waliotoroka wanatuhumiwa na mauaji
ya aliyekuwa mwenyekiti wa chadema ambapo waliotoroka ni wawili huku
wanne wakibakia magereza
Awali
wakati akihutubia wananchi wa kata ya daraja mbili Nassari alisema kuwa
kamwe hawatakaa kimya kutokana na filamu hiyo ya kutoroka kwa mahabusu
hao

Lema akimnadi mgombea udiwani kata ya daraja mbili Prosper Msofe
Hata
hivyo aliweka wazi kuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani
wanauhakika wa kuibwaga vibaya CCM kwa madai kuwa Arusha ni kisima cha
Mabadiliko
Katika
hatua nyingine Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Kamanda
Godbless Lema ametamba chadema kushinda katika uchaguzi mdogo wa udiwani
katika kata ya Daraja mbili Mkoani Arusha sanjari na maeno mengine hapa
Nchini

Kamanda Ephata Nanyaro Mh.Diwani kata ya Levolosi jijini Arusha akihutubia jukwaani
Wakati
akimnadi mgombea Udiwani wa kata hiyo anayefahamika kwa jina la Prosper
Msofe,Lema alisema kuwa wanauhakika na mgombea wao kupita kwa
asilimia100% katika uchaguzi huo
“Eee Mwenyenzi Mungu tunashukuru tumeshinda katika uchaguzi huu wa daraja mbili Ameni”Lema alianza kwa sala

Emmanuel Zachariah maarufu kama baba boni akihutubia mara baada ya kuvua gamba na kuvaa gwanda
Lema
alitoa tahadhari kwa baadhi ya watu waliomtumia sms kuwa mgombea huyo
hakubaliki kutokana na yeye kumiliki gorofa na kudai kuwa chama cha
chadema hakiamini katika umaskini na ndio sababu kubwa ya wao kupiga
vita umaskini
“Tuanahitaji
kila mtu hapa afanikiwe,,na umaskini sio uhadilifu na tunapiga vita
umaskini usiku na mchana na hatuwezi kuwa na chama kinachojisifia
nyundo na jembe wakati watu wanalima kwa trekta huku wakimwagilia kwa
maji ya chini”alisema Lema
Alibainisha
kuwa umaskini unaendelea kuwakandamiza wananchi na leo hii umri wa
kuishi mtanzania umeshuka kutoka miaka 70 hadi 45 kutokana na watu
kuishi katika mazingira magumu na kuwataka wananchi wapige vita umaskini
hata kwa kuuza figo zao
Pia
katika hatua nyingine alimtaka mgombea udiwani kutumia umbo lake la
ubaunsa kuhakikisha ndani ya halmashauri anatumia umbo lake kucheza na
wezi huku akimuonya endapo ataota pembe kwa kukiuka taratibu za chama
basi watamfuta kamati kuu na uchaguzi kurudiwa upya
“Chadema
haipendwi ubaunsa,kitambi na kombati inapendwa kazi ya kupigania
wanyonge na kama utaleta mauzauza basi tutakupiga chini kama ilivyokuwa
kwa Bayo,Mala na wenzake”alisema kamanda Lema
Kutokana
na hilo umati mkubwa wa wafuasi hao ulishangilia kwa sauti ya juu huku
wakimpongeza Lema kwa ushujaa wake huku wakipiga pipoooz power ndani ya
viwanja hivyo vya shule ya daraja mbili Mkoani Arusha
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia