
Meneja mahusiano wa shirika la Hifadhi ya Taifa(TANAPA)Pascal Shelutete akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
Shirika la
Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA)limezindua tuzo maalumu kwa waandishi
wa habari hapa Nchini ijulikanayo kama(TANAPA Media Awards 2012)katika
maeneo ya uhifadhi pamoja na Utalii wa ndani lengo ikiwa nikuongeza
uelewa juu ya wananchi kuhifadhi maeno ya hifadhi
Meneja
mahusiano wa shirika hilo Pascal Shelutete katika uzinduzi huo
alisema kuwa kwa mwaka huu wa 2012 watatoa tuzo kwa waandishi wa habari
watakao kuwa wameandika habari zitakazo saidia kuongeza uelewa kwa
wananchi juu ya kuhifadhi wa maeneo yaliyotengwa kama hifadhi za taifa
Alisema kuwa
wanahabari watakao jitoa kwa dhati kwa kuandaa vipindi,makala maalum
zinazohamasisha juu ya utunzwaji wa maeneo ya hifadhi za taifa
watatambua mchango wao kwa kutoa tuzo kama njia ya kuhamasisha waendelee
kuwaelimisha Watanzania,hususani wanaoishi jirani na hifadhi hizo kwa
kutambua umuhimu wa maeneo hayo
“Wanaishi
jirani na hifadhi hizo watapata uelewa mkubwa wa kuacha kuvamia maeneo
ya hifadhi,kuingiza mifugo ndani ya hifadhi,,kwa sababu ushirikianio
baina ya shirika na wananchi hao ndio utakao saidia kuhakikisha hifadhi
hizo zinaendelea kudumu”alisema Shelutete
Aliongeza kuwa
katika eneo la pili ambalo ni utalii wa ndani unaonyesha kuwa muamko wa
watanzania kutembelea maeneo hayo ya hifadhi umekuwa ni wa chini sana
huku akidai kuwa pengine ni jamii kutotambua maeneo hayo ya hifadhi
pamoja na utamaduni uliojengeka kuwa wanaotakiwa kutembelea hifadhi hizo
ni wageni kutoka nje tu
Alibainisha
kuwa Mtanzania anawajibu wa kutembelea hifadhi hizo kwa kuona rasilimali
zilizopo katika maeneo mbalimbali ya Tanznia
Aidha alisema
kuwa vipindi hivyo pamoja na makala hizo zitakazo andaliwa na wanahabari
hapa nchini ziwe za kuibua au kuanisha vivutio vilivyopo katika maeneo
yaliyotengwa kama hifadhi za taifa pamoja na kuhamasisha watanzania
kuona umuhimu wa kutembelea vivutio hivyo
Katika
shindano hilo kutakuwepo na vipengele vitatu ambavyo ni
Redio,Televisheni na Magazeti ambapo katika eneo hilo atapatikana
mshindi wa kwanza hadi wa tatu hivyo kufanya washindi kwa ujumla kuwa
kumi na nane
Washindi
katika mchakato huo mshindi wa tatu katika kila eneo atajinyakulia pesa
tasilimu shilingi500,000 pamoja na cheti huku wa pili akipata
sh.shilingi 1,000,000 na cheti pamoja na ngao,mshindi wa kwanza ataibuka
na kitita ta shilingi 1,500,000 ,cheti,ngao pamoja na safari ya
kujifunza maswala ya utalii ya uhifadhi katika nchi za SADC
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia