Uongozi wa mfuko wa jamii wa
pensheni( PPF) na mifuko mingine hapa nchini imepatiwa changamoto ya
kuhakikisha kuwa wanafanya utafiti wa kina ili kubaini fursa ya kupata
wananchama wapya kutoka katika sekta isiyo rasmi.

Mgani rasmi Bi.Saad Mkuya akimkabidhi zawadi mshindi katika mkutano huu
Akizungumza wakati wa kufungua
mkutano wa 22 wa mwaka wa wananchama wa mfuko wa pesheni wa (PPF) na
wadau wengine wa hifadhi ya jamii jana jijini Arusha Naibu Waziri wa
Fedha Bi.Saada Mkuya Saalum alisema kuwa ni vyema mifuko hiyo ikafanya
utafiti ili kubainin njia madhubuti za kuongeza wananchama hao wapya.
Bi.Mkuya alisema kuwa sekta
isiyo rasmi imekuwa ikikua kwa kasi kubwa na hivyo kuajiri watu wengi
hivyo ni vyema kutumia matokeo ya utafiti zitakazofanyika na kuchukua
hatua zinazostahili za kuhakikisha wananchama waliopo katika sekta hiyo
isiyo rasmi nao wanajiunga na kuchangia mifuko hiyo.
“Naomba nitoe rai yangu kwenu
Uongozi wa mfuko wa PPF na wengine mfanye utafiti ili kubaini njia
mbadala za kupata wananchama wapya katika sekta isiyo rasmi kwa kuwa
inakuwa kwa kasi hivyo mkiwapata hawa kupitia utafiti wenu kitawasaidia
kupata michango na idadi ya wananchama itabadilika.”alisema Bi.Mkuya
Aidha alisisitiza kuwa maazimio
ya mkuatabno huo yawe dira katika kutekeleza majukum ya kuhakikisha
kuwa mifuko ya hifaddhi ya jamii nchini ionakuwa kichocheo cha
maendeleoya jamii na uchumi wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
mfuko wa PPF bw.Willium Urio alisema kuwa ifuko ya hifadhi ya jamii ni
kichocheo cha uchumiwa nchi kutokana na uwekezaji ambao unafanywa na
mifuko hiyo ikiwa ni pamoja na huduma nyingine mbalimbali za kijamii.
Bw.Williuma alisema kuwa
mkutano huo utaambatana na uopimaji wa hiari wa magonjwa mbalimbali kama
vile kisukari,virusi vya ugonjwa wa ukimwi,shinikizo la damu na uzito.
Pia
alionngeza kuwa wananchama wa mfuko huo watapata fursa ya kutembelea
mojawapo ya mbuga za wanyama hapa nchini “Tarangire”ili kujionea mambo
mbaklimbali yaliyopo katika mbuga hiyo ikiwa ni kuhimiza utalii wa
ndani.
Naye mwenyekiti wa bodi wa
mfuko huo Dkt.Adolf Faustine Mkenda alisema kuwa kiwango kimekuwa
kikiongezeka ambapo mfuko umeendelea na uwekezaji katika vitega uchumi
mbalimbali ambapo jumla y sh.bilioni 837.6 ziliwekezwa kufikia mwishoni
mwa mwaka 2011 ukilinganisha na shilingi 672.2 bilioni mwishoni mwa
mwaka 2010.
Hata hivyo alifafanua kuwa
mapato ya yatokanayo na uwekezaji yalipanda kwa asilimia 110 kutoka
shilingi 43.45 bil. Zilizopatikana katika mwaka 2010 hadi kufikia jumla
ya sh.91.38 bil. Zilizopatikana mwaka 2011 katika kipindi hicho cha
January hadi Juni mwaka 2012 mapato yatokanayo na uwekezaji yamefikia
jumla ya sh.47.714 bilioni kati ya lengo la sh.47.71 bil. Kwa kipindi
hicho.
Mkutano huo unaendelea katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa (AICC) uliopo jijini Arusha
uanatarajiwa kumalizika rasmi tarehe 13 october ambapo pia
umeshirikisha wadau wa mifuko ya hifadhi kutoka nchi ya
Zambia,Burundi,Rwanda na Afrika Kusini na wenyeji Tanzania.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia